Na Florence Majani, Mwananchi
Posted Ijumaa,Novemba8 2013 saa 10:40 AM
Posted Ijumaa,Novemba8 2013 saa 10:40 AM
Kwa ufupi
- Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mtaalamu wa waathirika wa dawa za kulevya, Augustine Godman anasema, magonjwa ya akili kwa ujumla wake yanaweza kuzidi 1,886 lakini yapo yale ya ngono ambayo pengine yana changamoto lukuki kwa mwanadamu hasa Watanzania wasiofahamu kuwa ni magonjwa ya akili.
Huenda tumewaona wengi wao kama mashujaa, vijana wa kisasa au hata dada zetu wanaokwenda na wakati, kumbe ni wagonjwa wa akili.
Unasikiliza taarifa ya habari jioni. Unasikia
kuwa, mwanamume amembaka mtoto wa miezi mitatu. Unaihoji nafsi yako… ni
jambo gani lililosababisha akafanya ukatili huo? Je, ni tamaa kali ya
ngono?
Wengine hudhani ni kisasi au imani za kishirikina na kwamba wahusika wametumwa.
Huu ni upotoshaji, lakini ukweli ni kuwa hayo ni
magonjwa ya akili ya ngono ambayo yanawakumba asilimia 35 au zaidi ya
Watanzania wote.
Watanzania hawa wanaugua magonjwa haya kwa wakati
mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kijamii, kiuchumi na migogoro
katika familia na katika uhusiano.
Watu wenye magonjwa haya, si lazima watembee wakiokota makopo, kuvua nguo au kuwa na nywele ambazo hazijachanwa.
Hawa ni watu wa kawaida ambao tunafanya nao kazi, wenye uwezo mkubwa katika taaluma au pengine ni wazazi au hata walezi.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mtaalamu wa
waathirika wa dawa za kulevya, Augustine Godman anasema, magonjwa ya
akili kwa ujumla wake yanaweza kuzidi 1,886 lakini yapo yale ya ngono
ambayo pengine yana changamoto lukuki kwa mwanadamu hasa Watanzania
wasiofahamu kuwa ni magonjwa ya akili.
Dk Godman anafafanua kuwa magonjwa ya akili ya
ngono kuwa ni yale yanayohusisha athari , upungufu au mparaganyiko au
vitu visivyo vya kawaida katika tendo la ngono.
“Mtu anaweza kuwa na matatizo ya kihisia au ya
kisaikolojia au vya kitabia katika suala la ngono na huweza kusababisha
madhara au kutopata mafanikio,” anasema Dk Godman
Daktari huyu ambaye amewahi pia kufundisha Chuo
Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), kitengo cha magonjwa ya
akili anasema watu wengi wana magonjwa ya akili ya ngono, lakini
hawajui kama ni magonjwa na wanaendelea kuishi hivyo hivyo wakidhani
ndivyo walivyo na baadhi wakipata matatizo katika jamii, wengine
kufungwa jela au kupigwa kutokana na tabia hizo.
Mara nyingi tumekuwa tukiona wanawake wanavaa mavazi ya nusu uchi, wakizianika nje sehemu kubwa za miili yao.
Tabia hizo ambazo pengine huweza kuigwa na wengine ni miongoni
mwa magonjwa ya akili ya ngono kwani watu wanaopenda kufanya hivyo
hujisikia raha na amani watu baki au wageni wenye jinsi tofauti
wanapoyaangalia maungo yao na kushtuka.
“Kwa kitaalamu, ugonjwa wa akili ya ngono wa
kupenda kuacha mwili wazi unaitwa ‘exhibitionism’ ambapo mtu huweza
kuamua kuacha maziwa, mapaja au kwa wanaume kuvaa suruali inayoelekea
kuanguka kutoka maungoni,” anasema
Anasema, watu aina hii hutosheka kimapenzi mara tu
wanapoona wanaume au wanawake wengine wameyaona maungo yao. Hata
hivyo, anasisitiza kuwa hutosheka pale tu watu wageni wanapoyaona maungo
yao.
Mhadhiri wa Sosiolojia, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Dk Thomas Ndaluka anasema, baadhi ya magonjwa haya
yanasababishwa na historia ya mtu.
Anasema hata hivyo mparaganyiko kama ule wa
kupenda kuacha maungo wazi, unaambukiza kwa maana ya kuwa, anayeanza
kufanya hivyo ni mgonjwa wa akili na matokeo yake wengine wanaiga.
Ubakaji wa watoto wachanga
Wengi wamekuwa wakihusisha ugonjwa huu na imani za
kishirikiana, lakini ukweli ni kuwa, wale wanaowabaka watoto wadogo au
kuwalawiti wana matatizo ya akili ambayo kitaalamu yanaitwa pedophilia
(paedophilia).
“Katika hali ya kawaida si rahisi mtu mzima akamtamani kimapenzi mtoto wa miezi mitatu,” anasema mtaalamu huyo.
Ugonjwa huu unatokea pale mtu anapokuwa na hali ya kupata raha ya ngono kwa watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano.
“Watoto wa jinsi zote huweza kuathiriwa na tatizo
hili. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kuamua kumuingilia mtoto au tu
kuamua kumchezea via vyake vya uzazi,” anasema Dk Godman.
Mhadhiri wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Dk Kitila Mkumbo anasema sababu kuu za maradhi hayo ya akili ni
pamoja na mazingira ya mtu wakati wa balehe, aliambiwa nini kuhusu tendo
la ndoa na makuzi yake kwa jumla.
Endelea kusoma habari hii: mwananchi
“Kwa mfano inategemea kijana anaambiwa nini wakati wa balehe au
yeye mwenyewe anaelewa nini maana ya tendo hilo” anaeleza Dk Mkumbo.
Anatoa mfano kuwa, wapo baadhi ya wanaume wanaamini au kufananisha kila shimo na uke.
“Huu ni ugonjwa mkubwa sana. Ndiyo maana utasikia
mtu kambaka mbuzi. Yeye anaamini kila shimo linaweza kutumika kama uke”,
anasema
Anafafanua kuwa magonjwa mengi ya akili ya ngono hujitokeza wakati wa balehe na hukua kadri mtu anavyokosa matibabu.
Yapo matukio kadhaa yaliyowahi kutokea hapa nchini yanayoeleza watu waliowabaka watoto wadogo.
Kwa mfano, Desemba 2012, Yakobo Raymond
alifikishwa mahakamani huko wilayani Muheza, Mkoani Tanga kwa tuhuma za
kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu.
Pia, huko mkoani Arusha, mwezi Januari mwaka jana,
David Samweli mkazi wa Moivaro Wilaya ya Arumeru, aliwabaka watoto
wawili wa kike wa jirani yake na mtoto wake wa kumzaa kwa nyakati
tofauti chumbani kwake.
Licha ya matukio kama haya kuripotiwa zaidi kwa
wanaume wenye tabia hii, Dk Godman anasema wapo wanawake ambao pia
huwabaka watoto wadogo wa kiume.
“Mwanamke anaweza kumvua nguo mtoto mdogo na
kuanza kumshikashika tu, hapo huwa amepata raha yake. Lakini pia
anaweza kuamua kumwacha mtoto akiwa uchi,” anasema
Mtu mwenye ugonjwa huu humrubuni mtoto kwa vitu
vidogo vidogo ili ampende na kumweka karibu naye na wakati mwingine
baada ya kumfanyia vitendo hivyo humtishia kuwa akisema, atamdhuru.
Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa, wapo watu
katika nchi zilizoendelea ambao huasili watoto, kisha kuwatendea
vitendo hivi vya upedofilia................................
Endelea kusoma habari hii: mwananchi