Na Joseph Zablon na Pamela Chilongola, Mwananchi
Posted Jumatano,Novemba13 2013 saa 9:7 AM
Posted Jumatano,Novemba13 2013 saa 9:7 AM
Kwa ufupi
Akizungumza kwa niaba ya familia ya Samizi
nyumbani kwake, Tegeta Dar es Salaam, Katibu Mkuu msataafu wa CCM, Yusuf
Makamba alisema maziko yatafanyika leo baada ya swala ya adhuhuri.
Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuongoza maziko ya Mkuu wa zamani wa
Wilaya mbalimbali nchini, Mussa Samizi aliyefariki Dar es Salaam, juzi.
Akizungumza kwa niaba ya familia ya Samizi
nyumbani kwake, Tegeta Dar es Salaam, Katibu Mkuu msataafu wa CCM, Yusuf
Makamba alisema maziko yatafanyika leo baada ya swala ya adhuhuri.
Makamba alisema, “Nilizungumza na Samizi muda
mfupi, baadaye nilipata simu kuwa mtu huyu amefariki... Wale mabwana
walipiga baada ya kuchukua simu yake na kuangalia mtu wa mwisho
kuzungumza naye.
“Baadaye ya kunieleza kuwa amefariki kwenye
daladala, nikawaambia wampeleke Hospitali ya Lugalo kwa ajili ya
taratibu nyingine... Kimsingi alikuwa anakwenda ofisi za TRA (Mamlaka ya
Mapato Tanzania).”
Enzi ya uhai wake, Samizi aliwahi kuwa Mkuu wa
Wilaya za Kasulu, Kigoma Mjini, Tabora, Handeni na Moshi mkoani
Kilimanjaro ambako alistaafu.
Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Habari Tanzania (Shihata) na
Shirika la Ujenzi wa Barabara (Mecco).
Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Camilus Wambura
alisema taarifa za msiba huo alipewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Jordan Rugimbana baada ya kutaka apewe ulinzi kwa ajili ya msiba huo.
“Mimi sina taarifa ya aliyekuwa mkuu wa wilaya
kufariki akiwa kwenye daladala, ninachojua alikuja Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni leo (jana) asubuhi ili nimpatie walinzi kwa ajili ya kwenda
nao kwenye msiba,” alisema Wambura.
Ilielezwa kwamba alikuwa anasumbuliwa na kisukari. Samizi ameacha mjane na watoto watatu.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI