Friday 8 November 2013

RIPOTI KAMILI:TIDO MHANDO AMUUMBUA MBUNGE ALIYESEMA ALIWAHI FANYA KAZI BBC KITENGO CHA PROPAGANDA

Mtangazaji/Mwandishi wa siku nyingi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania Tido Mhando ameyatoa ya moyoni kuhusu Mbunge mmoja wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambae hajapendezwa na mwenendo wake. 

Ishu ilianzia kwenye headline ya kuwasema Waandishi wa habari ambapo namkariri Tido akisema  ‘kuna wengine miongoni mwetu ambao wanachukua nafasi hizi kujaribu kutafuta njia za kujipenyeza ili waweze kujenga majina yao na kuharibu ukweli wa fani yetu, tunawafahamu baadhi yao.. kuna wengine wamefikia hatua hadi kuingia mjengoni na huko wanatamka maneno ambayo kwakweli huwezi kuamini kama walikua Waandishi wa habari’


‘Mfano kuna mwenzetu mmoja yuko pale (bungeni) na bahati mbaya kauli zake ni kutusema Waandishi wa habari kitu ambacho sidhani kama ni kweli, kwanza mwenyewe sielewi kama ni kweli kwamba aliwahi kuwa kwenye kitengo cha Propaganda BBC, nimekua BBC kwa miaka 20 nilikua kiongozi wake, hata siku moja sikuwahi kukiona kitengo hicho cha Propaganda…. wala si hivyo, sidhani kama yeye mwenyewe alishaeleza ukweli  kwamba alikua vipi pale BBC, ni wazi aeleze kwamba kweli aliwahi kuajiriwa na BBC au alichukuliwa tu kwenda kusoma habari, sasa kama kusoma habari ndio kujiita mwandishi wa habari basi inabidi aeleze’ – Tido

Kwa kumalizia, Tido amesema ‘na labda mwishoni aeleze ni kwanini hatimae aliamua kuondoka BBC, sasa kiasi hiki cha Makanjanja ambao tutawaruhusu waingie na hatimae kuwapa hali ambayo kwakweli inakua na maana potofu kwetu, hali hii inatuharibia na kamwe tusiwakubali watu hawa waingie wawe miongoni mwetu, watu hawa wameidhalilisha sana sekta ya habari na ni wajibu wetu kuhakikisha waandishi wote wana uwezo wa kweli kufanya kazi hii na pia tukubali kwamba endapo chombo cha habari au mwandishi amekosea, kuna vyombo ambavyo vimewekwa kufatilia makosa yetu’



SOURCE: KANDIRI HURU