Na Joyce Joliga, Mwananchi
Posted Jumanne,Novemba19 2013 saa 24:0 AM
Posted Jumanne,Novemba19 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Nape licha ya kukiandama Chadama alisikitika hakuna waziri wa kilimo aliyewahi kwenda mkoani Ruvuma.
Songea. Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nauye amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
kukifuta Chadema kwa madai kuwa, kimeshindwa kusimamia katiba yake kwa
kutofanya uchaguzi wa ndani zaidi ya miaka zaidi ya kumi.
Nape alisema chama hicho kimejaa viongozi waongo,
wapenda vurugu na wanaotaka kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha
Katiba Mpya na kwamba, wamesahau katiba iliyopo imedumu kwa miaka 50 na
haijawahi kuwagombanisha wananchi wala kuwavuruga.
Hata hivyo, jitihada za kumpata Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika kuzungumzia tuhuma hizo jana jioni
kwa simu yake haikufanikiwa.
Akihutubia wakazi wa Manispaa ya Songea jana, Nape
alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kukiagiza chama hicho kufanya
mkutano wa uchaguzi haraka kikigoma akifute na kwamba, asipofanya hivyo
wao wataendelea kumsema na kumchukulia hatua.
Aliongeza CCM kilifanya uchaguzi wake 2012 na
kupata viongozi wapya, lakini Chadema imeshindwa kusimamia katiba yake
ambayo ilipeleka kwa msajili wa vyama na kuisajili kwa kuivunja wao
wenyewe kwa kuendesha chama isivyo.
Nape alisema chama hicho hakifai kuongoza nchi, kwani kimeshindwa kusimamia katiba yake na kuifuata hakiwezi kuongoza wananchi.
“Kwa sababu Msajili wa Siasa ni mlezi wa vyama
vyote vya siasa ikiwamo Chadema, namuomba akiagize chama hicho kifanye
uchaguzi kwani wao wanajiita wanademokrasia wakati wanashindwa kufuata
demokrasia kwa vitendo,” alisema Nape.
Kuhusu malalamiko ya wananchi, Nape alisema
wananchi wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi wa Serikali
na kwamba, yana msingi kwani inasikitisha licha ya Ruvuma kuwa ni mkoa
unaolisha nchi, hakuna mawazili wa kilimo ambao wamefika mkoani hapa.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI