Na Dorothy Jebet,Mwananchi
Posted Jumatano,Novemba13 2013 saa 13:8 PM
Posted Jumatano,Novemba13 2013 saa 13:8 PM
Kwa ufupi
Upinzani umegundua kwamba Serikali ya Jubilee
imeanza kuonyesha kucha zake miezi michache baada ya kujifanya kwamba
inafuata sheria na kulinda Katiba. Ilifanya hivyo kwa kuteua Baraza la
Mawaziri inavyotakiwa kisheria, lakini sasa mambo yamebadilika.
“Tulionywa na Amerika kabla ya uchaguzi
kwamba tukiwachagua Uhuru na Ruto tungejuta na sasa tumejuta. Wakenya
milioni sita walimchagua Uhuru. Kweli sikio la kufa halisikii dawa.
Dalili ya mvua ni mawingu. Mawingu yanayofunika
anga la Kenya wakati huu yanaashiria kwamba mvua itakayonyesha
itasababisha mafuriko katika nyanja za kisiasa na kiuchumi.
Ni kwa sababu hii wote wanaojali hatima ya nchi
hawana budi kujitokeza kimasomaso ili kuona athari za vitendo vya
Serikali ya Jubilee kwa nchi na kutafuta jinsi ya kuepukana nazo.
Jukumu hili liko juu ya mabega ya vyama vya
upinzani haswa Muungano wa CORD unaoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu,
Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na wengine.
Ni wakati wa CORD kuonyesha kuwa haiwezi kusita
kueleza na kuihakiki Serikali ya Uhuru Kenyatta pia ni dhabiti na kwamba
viongozi wake watakuwa wanazungumza kwa sauti moja wanapoikosoa
Serikali.
Wengi walitarajia kwamba viongozi wa Cord
wangetengana baada ya uchaguzi mkuu, lakini Raila, Kalonzo Musyoka na
Moses Wetangula bado ni wanachama wa CORD.
Historia ya vyama vya kisiasa nchini inaonyesha
kwamba, viongozi huunda vyama kwa lengo la kushinda uchaguzi lakini
baada ya miezi michache vyama hivyo husambaratika.
Kwa mfano, kiongozi wa United Democratic From
(UDF), Musalia Mudavadi anajitayarisha kujiunga na Serikali ya Uhuru
kama waziri. Gazeti moja la kila siku limenukuliwa likiripoti kwamba,
Mudavadi hivi karibuni ataingizwa kwenye serikali.
Tatizo nini?
Upinzani umegundua kwamba Serikali ya Jubilee
imeanza kuonyesha kucha zake miezi michache baada ya kujifanya kwamba
inafuata sheria na kulinda Katiba. Ilifanya hivyo kwa kuteua Baraza la
Mawaziri inavyotakiwa kisheria, lakini sasa mambo yamebadilika.
Uhuru na Makamu wake,William Ruto, wameonyesha
kuwa hawajali lolote zuri linaloiweka Kenya kwenye jukwaa la mataifa
yanayowalinda wananchi wake. Kwa wiki moja iliyopita, Upande wa Serikali
bungeni umepitisha miswada miwili inayorudisha nyuma hatua nzuri
zilizokuwa zimepigwa.
Kumekuwa na kilio kikuu kutoka kwa Wakenya kuhusu
hatua ya Serikali kutaka kuzima uhuru wa wanahabari na pia kukata msaada
kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka kwa mashirika ya maendeleo ya
nchi za Ulaya na Magharibi.
Endelea kusoma habari hii: mwananchi
Endelea kusoma habari hii: mwananchi