Siku
chache baada ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kutoa msimamo
wa Tanzania kutokujitoa katika jumuiya ya Afrika mashariki waziri wa
mambo ya nje wa Kenya amempongeza rais Jakaya Kikwete na kusema kuwa
hatua hiyo itaimarisha zaidi uhusiano wa juimuiya hiyo.
Kauli hiyo imekuja siku tatu baada ya raisi wa
jamuhuri ya muungano wa Tanzania kulihutubia bunge na kueleza msimamo
huo ambapo waziri wa mambo ya nje wa Kenya Mh. Amina Mohamed aliekuja
Tanzania kwa lengo la kumpongeza raisi amesema nchi yake imekuwa
ikufanya baadhi ya maamuzi yanayohusu jumuiya bila kuishirikisha
Tanzania kwa kutokujua wanakiukwaji taratibu za jumuiya na kwamba
kunzaia sasa watafuata taratibu zote ili kuhakikisha jumuiya hiyo
haitavunjika pamoja na uhusiano baina nchi uwanachama.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Mh. Bernadi Membe mbali na
kupongeza hatua ya waziri wa Kenya amefafanua msimamo wa Tanzania kuhusu
swala la ardhi pamoja na shirikisho la haraka katika jumuiya ya Afrika
mashariki utaendelea kuwa palepale na kuwa swala la shirikisho
linahitaji muda wa kujadiliwa ili kila nchi uanachama waweze
kujiridhisha.
Wakati huo huo mwenyekiti wa chama cha wananchi
-CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amesema hatua ya raisi Kikwete ni ya
kizalendo na kwamba kuna haja ya wachambuzi wa mambo ya uhusiano wa
kimataifa kuchambua kwa kina ili kubaini chanzo cha tatizo
lililojitokeza katika jumuiya hiyo ili kuhakikisha haitatokea tena na
uhusiano baina ya nchi uanachama unaimarika.
SOURCE; ITV