Saturday 2 November 2013

Pinda na Kagasheki wajiuzulu- Wabunge

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia), akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi (wa pili kushoto), mara baada ya kuahirishwa kwa Bunge jana mchana. Wabunge walicharuka na kukemea serikali kushindwa kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima na kuendesha vibaya Operesheni Tokomeza Ujangili nchini. Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David na kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.