Sunday 3 November 2013

RIPOTI KAMILI: BAADA YA MADAWA YA KULEVYA, UHAMIAJI HALAMU NA SASA NI UJANGILI

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki (wa pili kushoto), akiwa ameshika pembe za ndovu zilizokatwa jana jijini Dar es Salaam toka kwa raia watatu wa China katika operesheni aliyoiongoza.PICHA|FILE  


 

  Pamoja na kwamba malalamiko dhidi ya operesheni hiyo yanatakiwa kushughulikiwa na ukiukwaji huo wa haki za binadamu kukomeshwa, madai hayo yanatakiwa kutazamwa kwa umakini kulingana na unyeti wa tukio na mazingira yake.PICHA|EMMANUEL HERMAN  

 Alisema thamani ya wanyama wote waliotoroshwa ilikuwa ni Sh170.5 milioni na kwamba twiga hao wanne kila mmoja alikuwa na thamani ya Dola 10,000 za Marekani sawa Sh60 milioni za Tanzania. PICHA|MAKTABA 

Tanzania nchi yenye kusifika kwa amani iliyodumu miaka mingi barani Africa haishi kuwa na vituko. Watanzania walio wengi mara nyingi husema "Tanzania inashi kwa matukio" na watu wake ni rahisi sana kusahau yaliyotokea jana na kuanza kushughulikia ya leo. Msemo huu unaweza kudhibitishwa na matukio ya hivi karibuni.

Ambapo kumekuwa na mtukio ya Madawa ya kulevya mara kwa mara. Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa waziri wa Uchukuzi aliingilia kati suala hili na kuwasha moto mkubwa na chini kutikisika juu ya suala la madawa ya kulevya. 

Baada ya siku kadhaa tulishuhudia watu wengi wakikamatwa sehemu mbali mbali za nchi. Hili lilipokelewa na kwa furaha na wananchi wengi hapa Tanzania. Kimsingi watanzania walio wengi wanatamani viongozi kama waziri wa Uchukuzi. 

Vyombo vya habari vilikuwa mstari wa mbele kulipoti matukio hayo lakini ni vyombo hivyo hivyo vinavyotumika kubadili upepo wa yale mambo muhimu na wahusika wake. 

Miezi ikapita, kisha suala ya uhamiaji haramu likashika kasi na vyombo vya habari vikaendelea  kutuhabarisha na kuondoa akili zetu katika suala zima la madawa ya kulevya. Nadhani hili limetoa haueni kwa wazee wa madawa kujipanga upya. Sasa ikawa ni uhamihaji haramu wengi wakaupongeza. Lakini nani asiyejua kuwa kuna watu wasio na hatia wamepoteza maisha na wengine kupora mifugo yao pasipo kufuata sheria za chi?

Hapa ukweli haupingiki kuwa watanzania ni watu wa matukio maana mpaka sasa hakuna ambaye amehoji. Lakini je nani mwenywe uwezo wa kuhoji ususani kwenye vyombo vya sheria na habari? Jibu la haraka ni wabunge na bunge zima. Hakuna mbunge ambaye mpaka sasa amehoji maendeleo ya operesheni ya madawa ya kulevya. 

Haya, nalicha hilo nirudi kwenye upepo wa leo. Mara hii ni Ujangili, kumekuwepo na timbwili timbwili la ujangili ambapo kikosi maarumu cha kupambana na ujangili kimefanya kazi kubwa ya kupambana na ujangiri. Kuanzia Dar es salaama mpaka Morogoro, Singida mpaka mara. Yote haya ni sehemu ya mipango ya serikali ya awamu ya nne. 

Kama kawaida, vyombo vya habari viemeendelea kutoa repoti na taarifa mbalimbali juu ya mapambano haya dhidi ya majangilli. Kuna taarifa za kupoteza askari wetu katika mapambano haya na pia wanachi wasio na hatia kupoteza maisha. 

Nitaambatanisha taarifa kutoka gazeti la Mwanachi juu ya taarifa za hivi karibuni juu ya upepo wa sasa wa mapambano juu ya ujangili. 

Natoa pongezi kwa Waziri wa Maliasili na pia kutoa pole kwa askari walipoteza maisha. Nalaani matukio ya kuuwawa wananchi wasio na atia yaliyo fanya na polisi  maana tafsiri kamili ya kulindanchi.

Natoa changamoto kwa wabunge wanao beza mpango huu maana nadhani lazima wajiangalie upya dhidi ya madai yao kwa Waziri mkuu na Waziri wa Maliasili. 

Shehena pembe za ndovu yakamatwa Dar

Na Goodluck Eliona, Mwananchi

Posted  Jumapili,Novemba3  2013  saa 10:14 AM
Kwa ufupi
Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar es Salaam.
Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.
Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung .
Raia hao wa China wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mingi wakifanya biashara ya kuingiza nchini vitunguu swaumu kutoka China na kusafirisha nje ya nchi makombe yanayopatikana baharini.
Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Kagasheki ambaye aliambatana na askari polisi na baadhi ya maofisa usalama alishuhudia shehena kubwa ya pembe za ndovu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba vyenye uzito wa kilo 50.
Mbali ya kushuhudia shehena ya pembe hizo, alionyeshwa gari maalumu aina ya Toyota Noah ambalo watuhumiwa hao hulitumia kutoa pembe porini na kuyaingiza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika eneo la tukio mara baada ya kuwakamata alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na matokeo ya Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imesitishwa na Serikali juzi baada ya wabunge kuilalamikia.
Waziri Kagasheki alisema kwamba katika harakati za kutaka kuwakamata watuhumiwa hao walitoa Sh30 milioni kwa ajili ya kujaribu kuwahonga askari.
“Walitaka kuwahonga askari ili wasikamatwe,” alisema huku akionyesha noti za fedha hizo.
Alisema wabunge wanaomtaka ajiuzulu kwa madai kwamba Operesheni Tokomeza Ujangili imesababisha mauaji ya watu na mifugo wanapoteza muda kwa kuwa mwenye mamlaka ya kumtoa ni Rais Jakaya Kikwete pekee.
“Sasa mimi nasema kunitoa haitakuwa rahisi anayeweza kunitoa ni yule aliyeniweka,” alisema.
Alisema ipo mikakati inayofanywa na baadhi ya wabunge kutaka kuwang’oa baadhi ya mawaziri kwa masilahi binafsi ya kisiasa.

“Itakuwa ni jambo la ajabu kwamba kila mtu akiingia madarakani wanataka atoke, watatolewa wangapi?” alihoji na kuongeza kuwa operesheni hiyo ni muhimu kwa ajili ya kunusuru tembo wasiishe.
Alisema kwamba ni kweli kuna baadhi ya dosari zimejitokeza kwenye operesheni ikiwamo kuuawa kwa baadhi ya mifugo, lakini siyo kwamba zoezi zima halina manufaa.
Kagasheki alisema kama kasi hii ya kuuawa kwa tembo itaachiwa iendelee baada ya miaka 10 tembo wote watakuwa wameisha nchini.
Alisema hataki kuona utawala wa Rais Kikwete ukiondoka madarakani ukiwa na lawama ya kuachia majangili wawamalize tembo.
Mmoja wa watuhumiwa hao, Huang Qin alisema shehena yote ya pembe za ndovu iliyokamatwa nyumbani kwake ilikuwa ikiletwa kidogo kidogo na rafiki yake ambaye hakumtaja jina.
Akiongea kwa Kiswahili Qin alisema: “Mimi hii si yangu, kichwa yangu mbovu. Rafiki yangu alileta hii (pembe) kidogo kidogo.”
Januari mwaka huu, Gazeti La Daily Mail la Uingereza liliripoti kwamba Serikali ya Kenya imekamata shehena ya vipande 638 vya pembe za ndovu ambavyo ni sawa tembo 320 waliouawa.
Mzigo huo wa tani mbili ulikuwa kwenye kontena la mawe ya urembo (marumaru) kutoka Tanzania.
Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa tani nne za pembe za ndovu zenye thamani ya Dola za Marekani 3.4 milioni sawa na takriban Sh5.4 bilioni zilikamatwa Hong Kong Oktoba 20, mwaka jana, huku ikielezwa kuwa meno hayo yalikamatwa yakisafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.
Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na pembe za ndovu yenye thamani ya Sh18.4 milioni yaliyotengenezwa kama bangili tayari kusafirisha kwenda nje ya nchi.

Jangili aua polisi, nao wamuua kwa risasi

Na Gasper Andrew, Mwananchi

Posted  Jumapili,Novemba3  2013  saa 1:3 AM
Kwa ufupi
Kundi hilo la majangili, linatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya biashara haramu ya nyara za Serikali. Tukio hilo lilitokea Oktoba 31 mwaka huu katika operesheni kutokomeza ujangili inayoendelea wilayani Manyoni.


Singida. Watu wawili akiwamo askari polisi wamekufa mkoani Singida katika tukio la kurushiana risasi na kundi la majangili katika Kitongoji cha Kirumbi, kilichoko katika Kijiji cha Kintanula wilayani Manyoni.
Kundi hilo la majangili, linatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya biashara haramu ya nyara za Serikali. Tukio hilo lilitokea Oktoba 31 mwaka huu katika operesheni kutokomeza ujangili inayoendelea wilayani Manyoni.
Askari aliyeuawa katika tukio hilo ametajwa kuwa ni mwenye namba G.9934 D/C Mgaka (26) wakati jangili ametambulika kuwa ni Selemani Kimpinde, mkazi wa kijiji hicho.
Akithibitisha tukio hilo baada ya kutembelea chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Taofiq, alisema baada ya askari huyo kumkamata jangili Seleman, walipanda gari na kuanza safari ya kwenda kuonyeshwa zilipo silaha aina ya SMG.
Alisema lakini walitembea umbali wa mita 100, kabla ya kufika kwenye eneo husika, askari hao waliamua kushuka kwenye gari na kuanza kutembea kwa miguu.
Taofiq alisema baada ya kufika kwenye eneo ambalo walitarajia kuonyeshwa silaha, alitokea jangili mwingine aliyekwenda kumpora askari silaha aliyokuwanayo.
“Wakati wa purukushani kati ya askari na jangili hilo lililomnyang’anya silaha, walijitokeza majangili wengine wawili na kumpiga risasi askari huyo. Baada ya askari kuanguka chini akiugulia maumivu, jangili huyo alianza kutimua mbio,” alisema.
Alisema jangili alikuwa hajawaona askari wengine waliokuwa wamejificha nje na kwamba waliposikia mlio wa risasi, askari aliyekuwa nyuma ya majangili hao alimpiga risasi jangili Kimpinde na kufa papohapo.

Waliokamatwa kwa ujangili Moshi kizimbani

Na Daniel Mjema, Mwananchi

Posted  Novemba2  2013  saa 9:18 AM
Kwa ufupi
Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani juzi ni pamoja na mfanyabiashara mashuhuri mwenye asili ya Kiarabu, Mohamed Hatiki (26), mkazi wa Kata ya Bondeni Mjini Moshi anayedaiwa kukutwa akimiliki silaha kadhaa bila vibali.
Dar es Salaam. Moshi. Watu wanne waliokamatwa na kikosi maalumu cha kupambana na ujangili kikiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za ujangili.
Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani juzi ni pamoja na mfanyabiashara mashuhuri mwenye asili ya Kiarabu, Mohamed Hatiki (26), mkazi wa Kata ya Bondeni Mjini Moshi anayedaiwa kukutwa akimiliki silaha kadhaa bila vibali.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmoja wa watuhumiwa ambaye ni fundi wa magari mkazi wa Pasua Mjini Moshi mwenye asili ya Kihindi, Mohamed Sadiq (67) alijikuta akianguka mahakamani baada ya kupata mshituko.
Sadiq anayedaiwa kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya Sh27.9 milioni, alianguka baada ya ndugu zake kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kukabidhi kortini fedha taslimu Sh14 milioni.
Ndugu zake hao walianza kumpepea kwa nguo mbalimbali na baada ya kesi kuahirishwa walitoka nje wakipaza sauti kwamba watakwenda kulalamika taasisi za haki za binadamu ndugu yao anaonewa.
Watuhumiwa hao walifikishwa mahamani na kusomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Omary Kibwana anayesaidiana na Mwendesha Mashtaka wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Rusticus Mahundi.

Makosa ya watuhumiwa hao ni uhujumu uchumi na pia ni kinyume cha kifungu cha 3 na 86 (1)(2)(3) cha sheria ya hifadhi Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.
Kwa upande wa Sadiq, anakabiliwa na mashtaka tisa yakiwemo ya kupatikana na Tumbili wawili.


Waliokamatwa kwa ujangili Moshi kizimbani

Na Daniel Mjema, Mwananchi

Posted  Novemba2  2013  saa 9:18 AM
Kwa ufupi
Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani juzi ni pamoja na mfanyabiashara mashuhuri mwenye asili ya Kiarabu, Mohamed Hatiki (26), mkazi wa Kata ya Bondeni Mjini Moshi anayedaiwa kukutwa akimiliki silaha kadhaa bila vibali.
Dar es Salaam. Moshi. Watu wanne waliokamatwa na kikosi maalumu cha kupambana na ujangili kikiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za ujangili.
Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani juzi ni pamoja na mfanyabiashara mashuhuri mwenye asili ya Kiarabu, Mohamed Hatiki (26), mkazi wa Kata ya Bondeni Mjini Moshi anayedaiwa kukutwa akimiliki silaha kadhaa bila vibali.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmoja wa watuhumiwa ambaye ni fundi wa magari mkazi wa Pasua Mjini Moshi mwenye asili ya Kihindi, Mohamed Sadiq (67) alijikuta akianguka mahakamani baada ya kupata mshituko.
Sadiq anayedaiwa kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya Sh27.9 milioni, alianguka baada ya ndugu zake kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kukabidhi kortini fedha taslimu Sh14 milioni.
Ndugu zake hao walianza kumpepea kwa nguo mbalimbali na baada ya kesi kuahirishwa walitoka nje wakipaza sauti kwamba watakwenda kulalamika taasisi za haki za binadamu ndugu yao anaonewa.
Watuhumiwa hao walifikishwa mahamani na kusomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Omary Kibwana anayesaidiana na Mwendesha Mashtaka wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Rusticus Mahundi.

Makosa ya watuhumiwa hao ni uhujumu uchumi na pia ni kinyume cha kifungu cha 3 na 86 (1)(2)(3) cha sheria ya hifadhi Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.
Kwa upande wa Sadiq, anakabiliwa na mashtaka tisa yakiwemo ya kupatikana na Tumbili wawili.

wengine wagoma kutiwa nguvuni

Na Waandishi wetu, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Novemba1  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Baada ya kukamatwa kwa madiwani hao juzi, jana kikosi hicho kilikwenda kufanya upekuzi katika nyumba zao.
Serengeti na Arusha. Jitihada za Kikosi Maalumu cha Kuzuia Ujangili, kuwakamata polisi wa Loliondo, ili kuunganishwa na madiwani watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro akiwemo mwenyekiti wao, juzi zilikwama.
Kukwama huko kulitokana na kuibuka kwa malumbano katika Kituo cha Polisi cha Loliondo.
Katika tukio hilo, risasi kadhaa zilipigwa hewani .
Hata hivyo, baada ya kushindwa kukamatwa kwa polisi hao (majina yanahifadhiwa) na askari wa kikosi kurejea kambini, maofisa wa juu wa operesheni, waliagiza kuwa, polisi wanaotuhumiwa wawekwe rumande taratibu za kipolisi zitakapokamilika.
“Tuna orodha ya baadhi polisi kuhusika na mtandao wa ujangili, tutawafuata tena na kuwahoji,”alisema ofisa mmoja.
Madiwani na mwenyekiti wa kijiji mbaroni.
Baada ya kukamatwa kwa madiwani hao juzi, jana kikosi hicho kilikwenda kufanya upekuzi katika nyumba zao.
Habari kutoka katika Wilaya za Ngorongoro zilisema madiwani hao walikamatwa wakiwa katika semina ya hali ya hewa iliyokuwa inafanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Kwa mujibu wa habari hizo madiwani hao wote ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alipoombwa kuzungumzia kukamatwa kwa madiwani hao, Diwani wa Kata ya Enduleni, James Moringe, alisema huenda wanashikiliwa kwa mahojiano kwamba ana imani kuwa wataachiwa.
Wakati huohuo, Serikali imeshauriwa kuzifanyia marekebisho sheria ya ujangili.
Rai hiyo inatokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kukosekana kwa meno makali katika sheria hiyo hasa dhidi ya watu wanaokamatwa wakiwa na nyara za Serikali.


Imeelezwa kuwa hali hiyo inachangia katika ongezeko la matukio ya kuuawa kwa wanayamapori nchini.
Ushauri huo, ulitolewa juzi na Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori cha Kenya, Prof esa George Owiti, alipokuwa akitoa mada kwenye kongamano la kimataifa linalohusisha nchi zaidi ya 20 duniani.
Katika mkutano huo unaofanyika mkoani Kilimanjaro, Profesa Owiti alisema sheria hizo hazina makali kwa wahalifu.

“Ni vyema Tanzania ikaweka utaratibu wa kutumia teknolojia ya kisasa ya utambuzi wa wahalifu wa wanyamapori katika hifadhi kwa kuchukuliwa sampuli za wahalifu,” alisema Owiti.

Operesheni dhidi ya ujangili iungwe mkono

Na Mwananchi

Posted  Alhamisi,Oktoba31  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufup
Ni kweli, operesheni hiyo inatakiwa isiwe ya mateso, unyanyasaji, ukatili wala fursa ya ulipaji wa visasi, bali inatakiwa kuendeshwa kwa umakini, weledi na haki ili kuhakikisha kila mmoja anatendewa kadri ya matendo yake.

Kwa wiki kadhaa hapa nchini inaendeshwa operesheni ya kupambana na ujangili wa tembo na wanyama wengine chini ya kikosi maalumu kinachoundwa na maofisa kutoka katika vyombo vya dola, maarufu kwa jina la Operesheni Tokomeza.
Taarifa mbalimbali zimekuwa zikiripotiwa kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya kikosi hiki, ikiwamo watu mbalimbali kukamatwa wakidaiwa kuhusika na ujangili, hasa wa meno ya tembo, uhalifu ambao kwa siku za karibuni umeichafua sana nchi yetu kimataifa.
Watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa umma na wa kisiasa wamekamatwa katika maeneo ya Serengeti, Ngorongoro, Arusha, Ruaha, Iringa, Mahenge, Maswa, Meatu na kwingineko ambako pia, ushahidi wa aina tofauti umepatikana kuhusiana na vitendo vya ujangili.
Kukamatwa kwa watuhumiwa katika maeneo yote hayo ni ushahidi kwamba majangili wana mtandao mpana unaotumia nguvu za kifedha, kisiasa au za ulinzi wa dola kujiimarisha katika maeneo mengi ya nchi, na kuendelea kuhujumu maliasili za taifa.
Hata hivyo, pamoja na lengo zuri la operesheni hiyo, yapo madai ya kikosi hicho kutumia mabavu na ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwamo kupiga watu ovyo, kujeruhi na hata kuua watu kadhaa wanaotuhumiwa kujihusisha na ujangili.
Pamoja na kwamba malalamiko dhidi ya operesheni hiyo yanatakiwa kushughulikiwa na ukiukwaji huo wa haki za binadamu kukomeshwa, madai hayo yanatakiwa kutazamwa kwa umakini kulingana na unyeti wa tukio na mazingira yake.
Ni kweli, operesheni hiyo inatakiwa isiwe ya mateso, unyanyasaji, ukatili wala fursa ya ulipaji wa visasi, bali inatakiwa kuendeshwa kwa umakini, weledi na haki ili kuhakikisha kila mmoja anatendewa kadri ya matendo yake.
Tunatambua kuwa operesheni yoyote inayowahusisha watu wazito inakuwa na changamoto na vikwazo vingi, hali inayowasukuma hata wabunge kuanza kushinikiza Serikali kutoa orodha ya vigogo wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya ujangili.
Kwa mujibu wa madai ya wabunge hao na taarifa za vyombo vya habari, biashara hiyo haramu inawahusisha baadhi ya wabunge, mawaziri, watumishi wa Serikali na maofisa katika vyombo vya dola.
Jeshi la Polisi limetajwa kuongoza miongoni mwa makundi manne ya majeshi, ambayo watumishi wake wamekamatwa wakijihusisha na ujangili katika matukio saba ya ujangili. Wengine ni kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Magereza.
Mathalan, kwa jinsi tatizo hilo lilivyo kubwa, katika matukio ya karibuni yaliyohusisha maofisa wa vyombo vya dola, jumla ya meno ya tembo 686 yaliyotokana na kuuawa kwa tembo 343 yalikamatwa, na vipande vingine 447 vilipatikana.
Kwenye operesheni ya namna hii ambayo Serikali imekiri kuwapo fununu za wanasiasa kuwa miongoni mwa majangili, ni lazima kuwepo vikwazo na shinikizo la kuizuia au kukwamisha, kwa vitisho au malalamiko ya umma kutoka kila kona ili kuhakikisha operesheni husika haifanikiwi.

Kutokana na hali hiyo, tunaunga mkono kauli ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha aliyoitia juzi bungeni akiwataka wanasiasa kuacha kushikiza kwa kutumia nguvu zao za kisiasa, kusitishwa kwa operesheni hiyo kwa sababu yoyote, kwa kuwa tunaamini shughuli kama hii haiwezi kufanikiwa iwapo itaendeshwa kama lelemama.

‘Marubani waliotorosha twiga walitumia hati za kidiplomasia

Na Waandishi Wetu,Mwananchi

Posted  Alhamisi,Oktoba31  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Madai hayo yalitolewa jana na shahidi wa 13 katika kesi kuhusu utoroshaji wa wanyama hai kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro

Moshi na Dodoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, imeelezwa kuwa marubani wa ndege ya kijeshi ya Qatar, walitumika katika kutorosha twiga wanne kwenda Uarabuni na kwamba washtakiwa walikuwa na hati za kusafiria zenye hadhi ya kidiplomasia.
Shahidi wa 13, Prisca Sabugo ambaye ni Ofisa Uhamiaji, aliiambia mahakama juzi kuwa hati hizo hazikugongwa mihuri wala kupewa viza.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo, shahidi huyo alidai kuwa ndege hiyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) Novemba 24 mwaka 2011.
“Baada ya hiyo ndege ya jeshi kutua, alikuja wakala wao kutoka Kampuni ya Equity Aviation akaniletea Diplomatic Passport zao na akaniambia wamekuja kwa shughuli za utalii kwa siku tatu,” alisema.
Huku akiongozwa na mawakili wa Serikali, Evetha Mushi na Joseph Maugo, shahidi huyo alidai kuwa marubani na wafanyakazi wa ndege huwa hawapitii utaratibu wa kawaida wa kujaza fomu na kupewa viza. Alisema, tangu wageni hao waingie nchini kama watalii, hawakuwahi kuhojiwa na chombo chochote kuhusu kutogongwa mihuri kwenye hati zao.
Shahidi wa 12, Oscar Jullius ambaye ni Ofisa Wanyamapori, alidai kuwa vibali vilivyotumika kukamata wanyama hao vilikuwa vya kampuni mbili ambazo ni Ham Market na Luega Birds Traders.
Kwa mujibu wa shahidi huyo, vibali hivyo vilikuwa vya kumiliki nyara na si vya kukamata wanyamapori hai na kwamba yeye ndiye aliyeandika ripoti ya thamani ya wanyama hao.
Alisema thamani ya wanyama wote waliotoroshwa ilikuwa ni Sh170.5 milioni na kwamba twiga hao wanne kila mmoja alikuwa na thamani ya Dola 10,000 za Marekani sawa Sh60 milioni za Tanzania.
Alipoulizwa na mmoja wa mawakili wanaowatetea washtakiwa, Edmund Ngemela, kama vibali walivyokuwa navyo vilikuwa halali, alikiri kuwa vilikuwa halali na vilikuwa ni vya kumiliki nyara.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea Novemba 29 mwaka huu.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na raia wa Pakistan, Kamran Ahmed, Hawa Mang’unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu ambao wote wako nje kwa dhamana.
Katika hatua nyingine, madiwani watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro akiwamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo, wanashikiliwa na maofisa wa Kikosi cha Maalumu cha Kupambana na ujangili.

SOURCE: TASAO WRITER AND MWANANCHI