11 Oktoba, 2013 - Saa 13:09 GMT
Dereva mashuhuri mwanamke wa
mashindano ya langalanga Formula 1 Maria De Villota amepatikana
amefariki ndani ya chumba cha hoteli moja mjini Seville,Hispania.
Alipata majeraha mabaya kichwani na usoni baada ya kugongana na lorry katika jimbo la Cambridgeshire, Uingereza lakini aliruhusiwa kuanza tena kuendesha gari.
Iliarifiwa De Villota, binti wa dereva wa zamani wa mashindano ya Formula 1, Emilio De Villota,alikwenda Seville kuzindua kitabu kuhusu maisha yake.
Timu na madereva wa langalanga wameelezea kushtushwa kwao na msiba huo.
Jenson Button wa Uingereza amesema. "inasikitisha sana. Msichana huyu amekumbwa na masaibu mengi sana, kupita yale yanayowakumba watu wengi duniani. Ni habari zilizotushtuwa timu nzima na jamii nzima ya mbio za langalanga."
"tulimuona mwaka huu mjini Barcelona.Tukifanya kazi kwa wakfu wa kuwasaidia watoto na alikua wa kwanza kujitolea na kuwashawishi madereva wengi kujiunga nasi.Alikua akichangia mengi kwa jamii ."
CHANZO: BBC SWAHILI