Na Samwel Shita, Mwananchi
Posted Ijumaa,Oktoba11 2013 saa 12:8 PM
Posted Ijumaa,Oktoba11 2013 saa 12:8 PM
Kwa ufupi
Chumvi ni moja ya vitu vilivyomo katika maji ya
baharini, baada ya maji kuwa mvuke baada ya kupata joto, chumvi hubaki
kama vichangarawe vidogovidogo ambavyo huvunwa na kutumika.
Kila Jumapili ya mwisho ya mwezi Septemba kila mwaka huitwa Siku ya Moyo Duniani.
Lengo la siku hiyo ni kuwapa ufahamu watu kuhusu
magonjwa ya moyo ambayo ndiyo kwa kiasi kikubwa husababisha vifo kwa
wingi duniani. Tukio hili hulenga pia katika kuhamasisha njia za
kujikinga na zinazoweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa
hayo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO)
zinaonyesha kuwa mwaka 2005 peke yake palitokea vifo vya watu milioni
17.2 duniani kwa magonjwa ya moyo.
Hii ni asilimia 30 ya vifo vyote duniani huku
kina mama wakiongoza kwa kufa zaidi. Pia, kila mwaka katika vizazi hai
1,000, watoto wanane huzaliwa na matatizo ya moyo katika Tanzania.
Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya asilimia 20-30 ya watu wanaugua
magonjwa ya moyo.
Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2020 magonjwa ya
kuambukiza yatakuwa na uwiano sawa na magonjwa yasiyoambukiza, yaani
asilimia 50 kwa 50 kwa nchi za Afrika ambako kwa sasa vifo vingi
husababishwa na magonjwa ya kuambukizwa kama vile, malaria, kifua kikuu
na Ukimwi.
Hii ni kutokana na maendeleo ya kiuchumi ambayo
huambatana na magonjwa yasiyoambukiza kama vile, shinikizo la damu,
shambulizi la moyo, figo, kiharusi na kisukari. Siku ya magonjwa ya moyo
duniani inakwenda sambamba na matumizi ya kiungo muhimu kiletacho
ladha katika chakula, yaani chumvi.
Chumvi ni kitu chenye kihistoria duniani, tangu miaka milioni iliyopita chumvi imekuwapo na kutumika duniani.
Chumvi ni moja ya vitu vilivyomo katika maji ya
baharini, baada ya maji kuwa mvuke baada ya kupata joto, chumvi hubaki
kama vichangarawe vidogovidogo ambavyo huvunwa na kutumika.
Ukipita majumbani, hoteli zote, migahawa,
minadani, matamasha na mitaani vijiwe vya nyama choma utashuhudia ulaji
mkubwa wa chumvi. Watu hujimiminia chumvi katika chakula hata kama
chakula hicho kina chumvi. Wengi wao hawafahamu kama ulaji chumvi kwa
mtindo huo ni hatari kwa afya zao.
Tabia za kikemikali za chumvi
Chumvi ni muhimu sana kwa mwili wa mwanadamu kwa
kuwa huwa na kiambata kiitwacho sodium ambacho ni muhimu kwa kazi za
kimwili. Kikemikali, chumvi imebeba sodium chloride, ndani yake takriban
asilimia asilimia 40 kati ya hizo ni sodium.
SOMA ZAIDI: http://www.mwananchi.co.tz/Epuka-chumvi-za-mezani-kiafya/-/1596774/2027938/-/ns26qm/-/index.html
SOMA ZAIDI: http://www.mwananchi.co.tz/Epuka-chumvi-za-mezani-kiafya/-/1596774/2027938/-/ns26qm/-/index.html