Tuesday, 1 October 2013

Gaidi Samantha Lewthwaite kusakwa nchini

30th September 2013
Samantha Lewthwaite maarufu �mjane mweupe�
Jeshila Polisi linamsaka gaidi Samantha Lewthwaite maarufu ‘mjane mweupe’ anayedaiwa kupita mpaka wa Namanga mkoani Arusha kwenda Nairobi, Kenya ambako anahusishwa na tukio la ugaidi kwenye kengo la biashara la Westgate.

Mkuu wa Rasilimali watu wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye, alisema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha kipima joto kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV kilichokuwa kikijadili Watanzania wamejifunzi nini kuchukua hatua shambulio la ugaidi lililotokea Nairobi.

Andengenye alisema Jeshi la Polisi limejipanga kumsaka gaidi huyo ili asije akaleta uhalifu zaidi na kwamba ufuatiliaji wa mwanamke huyo hautafanywa kwenye mipaka bali hata ndani ya nchi.

“Tusitupie macho tu kwenue mipaka, magaidi wengine wanaweza wakawa wapo hapa ndani ya nchi hivyo tutatupia macho ndani, hivi sasa kuna programu ya kupeleka askari kila tarafa, wananchi watoe ushirikiano kwao ili kuimarisha ulinzi,” alisema.

Aliwaonya watu wanaosambaza ujumbe mfupi wa simu kutisha wananchi katika suala la ugaidi kwamba wakibainika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheriaa

Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ambaye pia ni Mtaalam wa Masuala ya Majanga, alisema taifa bado halijawekeza katika kukabiliana na majanga na ndiyo maana kukitokea tukio lolote hata kama ni dogo vyombo vya ulinzi na usalama vinachukua muda mrefu kulipatia ufumbuzi.

“Unakuta jeshi linakwenda kwenye tukio halina hata vitendea kazi, mfano ni tukio la kuporomoka kwa ghorofa ambako ilichukua siku nne kuondoa kifusi, wakati umefika taifa kuwekeza katika kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama,” alisema.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zisiangalie suala la kukuza uchumi baina ya nchi hizo bali ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama ni muhimu sana.

Alisema ili kuweza kuimarisha ulinzi wan chi kuna haja ya kuwatumia mabalozi wa nyumba kumi ambao badala ya kuwa upande wa chama wawe upande wa serikali ili waweze kuwajibika vizuri katika utendaji kazi.
CHANZO: NIPASHE