Idadi
kubwa ya malori mizigo yanayokwenda mikoani na nje ya nchi yamekwama
katika mizani ya Kibaha mkoani Pwani kwa muda kutokana na kubainika kuwa
na ongezeko kubwa la uzito wa mizigo lililo sababisha kutozwa kiwango
kikubwa cha fedha kuliko viwango vilivyokuwa vikitozwa awali.
Wakizungumza
na waandishi wa habari, madereva wa malori hayo wameilalamikia serikali
kuweka utaraibu mpya wa upimaji unaoonyesha kuwepo kwa uzito mkubwa na
tozo bila ya kutoa elimu kwa wamiliki na madereva wa malori hali
inayosababisha idadi kubwa ya malori kubainika kuwa na uzito mkubwa
tofauti vipimo vya siku zilizopita.
Aidha
Itv imeshuhudia malori yaliokuwa yamebeba gesi,mingine mafuta ya
petroli na mafuta mazito yakiwa pamoja na malori ya mizigo ndani ya eneo
la mizani hiyo hali ambayo ni hatari,ambapo wakizungumza na waandishi
wa habari baadhi ya madereva wamesema kwa mujibu wa taratibu magari hayo
yanatakiwa kutembea si zaidi ya masaa 12 na kusisitiza kusimama kwa
muda mrefu katika mizani hiyo kumesababisha kushindwa kufuata taratibu
za usafirishaji..
SOURCE. ITV-DAIMA