Sunday, 6 October 2013

Rais Kikwete kutengua miliki za ardhi ambazo haziendelezwi Kisarawe


Rais Jakaya Kikwete akiwa ziarani mkoa wa Pwani: Picha na Issa Michuzi Blog
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka wilaya ya Kisarawe kuwabana na ikiwezekana kumletea taarifa ili atengue miliki kwa wawekezaji waliohodhi ardhi maelfu ya ekari pasipo kuitumia na kuwaletea manufaa wananchi na badala yake kupanga  kukopea benki au kuuza kwa bei ya juu.

Rais ameyasema hayo leo wilayani Kisarawe baada ya kuhoji utoaji huo wa ardhi holela pasipo kuweka makubaliano jinsi watakavyozitumia ardhi hizo.

Kauli hiyo ilikuja baada ya rais kuhoji mwekezaji wa shamba la Sun Biofuel ambapo maafisa wa idara ya ardhi na mazingira Edfas Bayela na omari kijiji walipodai mwekezaji huyo amebadili ghafla kilimo cha mibono na kuamua kulima mihogo
Wakati huohuo rais aliyepo kwenye ziara ya mkoa wa Pwani alitumia fursa hiyo kufungua jengo la jipya na la kisasa la mahakama ya wilaya na kuahidi serikali kuenedelea jitihada zake za kuboresha huduma za mahakama na kuanzisha mfuko maalum.

Kabla ya uzinduzi huo jaji mkuu Chande Othman alimwambia rais jengo hilo limetumia jumla ya milioni 938 na samani za shilingi milioni 72,na kusema mkoa wa Pwani bado una tatizo la uchakavu wa majengo ya mahakama na kulazimika kuzifunga mahakama za mwanzo nne kwa uchakavu

SOURCE: ITV -DAIMA