Sunday 6 October 2013

Malasusa:Ni vema zikajengwa nyumba za ibada nyingi kuliko magereza

 Ikiwa ni  mfululizo  wa matukio  ya  kuchomwa   moto makanisa  na matukio mengine  yanayopelekea  uvunjifu  wa  amani  mkuu wa kanisa la  kiinjili la  Kilutheri  Tanzania Dk Alex Malasusa  ameongoza  ibada maalum  ya  ufunguzi   wa nyumba  ya ibada  ya usharika wa  Mabibo Exteral  jijini Dar es salaam  huku askari  wenye  silaha  za moto  wakiwa  nje  ya  jengo  hilo.

Itv ilifika  katika usharika huo na kuwasuhudia askari wenye silaha za moto  wakizunguka huku na huko katika jengo hilo na  gari
Mbili za polisi zikiwa zimeegesha pembeni mwa kanisa hilo ikiwemo landrover  ya  OCD Kimara   huku ibada ikiendelea  ndani.

Akizungumza katika  ibada hiyo Dk Malasusa  amesema  ni vyema  kama zingekuwa  zinajengwa nyumba  za ibada zaidi  badala ya  sasa yanavyojengwa  magereza  vile magereza  hayatoshi  kumbadilisha mtu  bali  mtu  ajengwe  kwa  imani  ajifunza   kuyataunza mazingira yanayomzunguka .

Naye mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa usharika huo  Bw Ayo Urassa amesema ujenzi wa kanisa hilo ulianza mwaka  1991  na hadi unakamilika umegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.

SOURCE: ITV