4 Novemba, 2013 - Saa 05:22 GMT
Wanajeshi wa serikali katika
Jmauhuri ya kidemokrasi ya Congo, wanashambulia ngome ya mwisho ya waasi
wa M23 katika maeneo ya milimani ,msituni Mashariki mwa nchi.
Mamia ya wakimbizi wanatoroka vita karibu na mpaka wa Mashariki mwa Congo na kuingia nchini Uganda.Kiongozi wa wapiganaji hao Mashariki mwa nchi ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita vyao na jeshi la serikali.
Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.
Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.
Mazungumzo ya amani yanafanywa mjini Kampala, Uganda.
SOURCE: BBC SWAHILI