Friday 1 November 2013

Makinda aamua ‘ugomvi’ baina ya Lukuvi, Abwao


Na Habel Chidawali na Sharon Sauwa,Mwananchi

Posted  Ijumaa,Novemba1  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema shida waliyonayo wananchi wa Isimani ni sawa na maeneo mengine nchini .


Dodoma. Spika wa Bunge, Anne Makinda jana aliingilia kati mvutano baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi baada ya kubanwa na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Chiku Abwao.
Hali hiyo ilijitokeza pale Lukuvi alipolazimika kutumia nafasi yake ya uwaziri kujibu swali la nyongeza lililoulizwa na Abwao kuhusu mpango wa serikali wa kufikisha maji Isimani. “Mheshimiwa Waziri, Jimbo la Isimani wananchi wake wana matatizo makubwa ya upatikanaji wa maji na wamekuwa na maisha magumu,hivyo wanahitaji msaada huo, je Serikali inatoa kauli gani kuhusu kuwasaidia wananchi hao,” aliuliza Abwao.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema shida waliyonayo wananchi wa Isimani ni sawa na maeneo mengine nchini .
Baada ya majibu hayo, Lukuvi alilazimika kusimama ghafla na kuwasha kipaza sauti,ili kusawazisha jibu la swali hilo ambalo lililenga moja kwa moja katika jimbo lake,Baadhi ya wabunge walianza kupiga kelele za kumtaka Lukuvi asizungumze kwa kuwa swali lilimlenga moja kwa moja.


SOURCE: MWANANCHI