Nafikiri sote tumeona tulokuwako Zanzibar na wale waliokuwa nje ya
Zanzibar ni matumaini yetu kuwa mmesikia juu ya sherehe kabambe
zitakazofanywa mwanzoni mwa mwaka 2014 kusherehekea miaka hamsini tokea
Mapinduzi ya Zanzibar yafanywe,moja katika mambo ambayo yatafanyika
katika kuadhimisha sherehe hizo ni ujengwaji wa mnara wa miaka hamsini
ya mapinduzi,mnara huu utajengwa michenzani karibu na maskani ya Mwembe
kisonge.
Hatujui mnara huu utagharimu kiasi gani lakini tunajua kuwa
utagharimu mamilioni ya shilingi ambazo serikali haina,lakini kwa vile
wazee wa CCM wameona ni kitu ambacho ni muhimu sana basi lazima
kifanyike,ijapokuwa kuna mengi ambayo yangeweza kufanywa kwa kutumia
pesa hizi lakini kwa sasa kwa mjibu wa SMZ mnara ndio jambo muhimu
kuliko yote.
Kwa sasa hivi mnara ni muhimu kuliko matibabu,wengi
wenu mna jamaa au mmetembelea marafiki au baadhi yenu nyie wenyewe
mmewahi kwenda kujaribu kupata huduma za afya katika Hospitali ya Mnazi
Mmoja na hali mmeiyona,kwa ufupi hali inasikitisha,hakuna cheti wala
dawa,kitanda kimoja wanalala baina ya wagonjwa wawili mpaka watatu,na
ukienda kwenye hio wodi ya wazazi ndio hakusemeki,hivi juzi hapa
tumemzika mwanamke kijana mbichi hafiki hata miaka 40,Allah amlaze
mahali pema na amsameh makosa yake,sisi tunafahamu kuwa kila mwanadamu
anakufa kwa ahadi lakini lazima kuwe kuna sababu na sababu ya ndugu yetu
aliefariki juzi mtoto wa Malindi bila ya shaka ulikuwa ni uzembe tena
uzembe wa hali ya juu,marehemu alitokwa na damu mpaka akafariki wakati
madaktari,ndugu,jamaa na wazazi wakikaa wanamuangalia bila ya kuweza
kusaidia,ati imefikia kiwango kuwa daktari anasema mie siwezi kufanya
kitu kwa sababu sina nyenzo za kufanyia kazi,sina gloves wala sina vifaa
vya upasuaji,kwa hio ilobakia mgonjwa jifie halafu tuseme Allah ndio
kaandika,hii ndio hali yetu ya mnazi mmoja,na lini umewahi kumuona
muheshimiwa wa serikali akaumwa akaenda kutibiwa mnazi mmoja?
Wakiumwa na
ukucha tu wanapanda ndege wanaelekea India,kwa sababu wao peke yao ndio
binaadamu sie raia sio watu na kwanini wajali kuhusu sisi raia wa
kawaida ambao hatuna mbele hatuna nyuma?Lakini bado tunaambiwa haya ndio
matunda ya mapinduzi,ati matibabu bure,wakati siku ambayo ukienda huko
spitali unatakiwa ununue kila kitu mwenyewe,sasa hayo matibabu bure
yametokea wapi?
Tuende kwenye shughuli za elimu,hamuwezi
kutudanganya na mtasema mnachotaka lakini takwimu zinaonesha kuwa
kiwango cha elimu kinazidi kuanguka siku hadi siku,kuna mashule chungu
nzima ambayo yamefunguliwa ya private ambayo hayana maana yoyote,shule
za serikali na za private zote ni sawa huwezi kutafautisha baina
yao,zote watoto wanafeli na hakuna anaejali,na nani atakaethamini elimu
ikiwa viongozi wa chama cha tawala CCM msemaji mkuu Borafya?mtu alokulia
kupiga ngoma za kiluo na bomu pamoja na kupika tende pale
mwembeshauri,leo mtu huyu kawa mkuu wa wilaya na moja kati ya watukanaji
mashuhuri wa chama cha CCM.
Je kweli umuhimu wa elimu utajulikana kwa
mtu kama huyu?Watoto wanakaa kwenye sakafu mashuleni,mwalimu ananunua
chaki zake mwenyewe,maisha yamepanda kiasi ambacho mwanafunzi anakwenda
shule mchana bado hajala,jinsi ya maisha yalivyokuwa magumu mzee mpaka
aikamate riziki basi saa kumi ya jioni je kweli haya ndio maendeleo
ambayo ya kusherehekea na kupoteza mapesa na kujenga mnara ambao
hautasaidia wala kuleta faida yoyote kwa mwananchi?
Sisi ni
watu wenye heshima zetu na siku zote tunaheshimu wakubwa zetu,mpaka pale
wakubwa zetu wanapoonesha kutotuheshimu sisi basi na sisi tunakuwa
hatuna heshima dhidi yao,kwa maana hio basi leo tunadiriki kuwaita
viongozi wetu wezi na pia wazembe wa tabia,Dr Sheni kama unasoma haya
utatusamehe lakini katika viongozi wewe humo wewe ni mzembe wa tabia na
mburuzwaji kama mbuzi ambae hataki kunywa maji,najua watu watasema kuwa
hatuna adabu lakini mpaka siku utakayo tuonesha kwamba unatujali basi
sisi kwetu heshima itakuwa sio muhimu,kumbuka kuwa heshima ni kitu cha
bure hatuna haja ya kununua.
Kumbuka kuwa hatujasahau maafa ya MV
SPICES wala MV SKAIG,mamia ya watu waliokufa kwa uzembe na hakuna hata
mzembe mmoja mpaka leo alokwenda ndani kubwa ulolifanya muheshimiwa
Raisi umeona umuondoshe Mustafa Jumbe bandarini na kumpeleka kwenye
idara nyengine kwa jinsi akili zenu zilivyojaa ukoko na ukosefu wa
uzalendo,na kwa jinsi mlivyokuwa hamna haya wala hamjui vibaya mmekula
mpaka pesa za mchango wa maafa hayo mpaka leo mayatima hawajalipwa
halafu mtu kama wewe pamoja na Sefu Iddi mna uso wa kusimama mbele yetu
na kusema nchi ina maendeleo?
Sisi hatufikirii hata kama hiyo maana ya
maendeleo mnajua,siasa za ujinga na upuuzi mmeuweka mbele nyinyi siku
zote chuki fitna na majungu ndio sera zenu,miaka hamsini baadae bado
tunazungumza kuhusu watu wa Pemba ati hawajashiriki mapinduzi?nani
anajali kama wapemba hawajashiriki?kwani watu wa Mwanza na kagera
walishiriki? na kwa taarifa yako Muheshimiwa Raisi kama hujui basi na
wewe ni mpemba au sijui umesahau hicho kitu?Au siasa na madaraka
yamekulevya?Kumbuka kuwa miaka kumi sio mingi kulikuwa na Komando hapa
alovunjia watu nyumba akajiona yeye mtoto wa Firauni sasa hivi yuko
wapi?
Tizama Mwenyezi Mungu alivyokuwa mkubwa yule yule maalim Seif
alotiwa ndani na Komando ndio kawa makamo wa raisi wakati Komando kabaki
taabani nafsi yake maji atiliwe kwenye blender,hivi ndio Allah
anavyofanya mambo yake,kwa vile wewe uko juu sisi tunakusubiri ushuke
manake mpanda ngazi lazima ashuke na kama unavyojua kushuka mchongoma
ndio ngoma kwa hio na sisi tunakusubiri na tushakaa mkao wa kula.
Mmekuwa kama hamjasoma hivi kweli mmeona nyie ni bora kwenda kujenga
mnara wa upuuzi wakati hata maji hayatoki majumbani,watu wamefanya
vibyongo kwa kuchota maji,juzi hapa kuna mzee mmoja wa CCM alituambia
maendeleo yapo kwa sababu sasa hivi baada ya watu kubeba masusu vichwani
na kuuza samaki sasa hivi wanatumia baskeli na vipikipiki,maendeleo
hayapimwi kwa vitu kama hivi,maendeleo yanapimwa kwa kipato,ajira,afya
elimu na mambo mengine.
Ingelikuwa bora mara elfu kumi kama
mngetumia pesa mkaenda kununua viti vya mashule au vitanda na madawa
hospitalini,lakini hamna haya wezi wakubwa uwanja wa ndege umekushindeni
pesa mmekula na sasa hivi hamjui la kufanya,nchi mmeifisidi,na mtu
akisema kweli mnamuweka ndani au mnamwagia tindi kali mlivyokuwa
madhalimu,mji unanuka,watu wanajijengea ovyo,majumba ya michenzani
makaro yanafoka,mataka kila chochoro lakini bado mna pesa za kujengea
mnara wa ujinga,sijui tuseme kwamba hamyaoni haya?Au basi mmekuwa
mambumbu na vyeo vimekufanyeni muyasahau yote haya?
Mashekhe
wetu mmewaweka ndani kisa ati wanahatarisha usalama,kwa taarifa yenu
mashekhe wetu hawajauwa mtu,wauwaji ni nyie mlouwa watu kwenye meli
zilizozama,na kweli hasa kama wewe Sheni mpenda haki mbona hujaenda
kukamata machangu doa kule bwawani usiku?Au wale sio majanga kwa
taifa?Tuna uhakika wale wanasambaza ukimwi je kati ya wale na mashekhe
nani hatari kwa taifa?Au umeamua kuyafumbia macho kwa sababu watu
walokuweka unawaogopa?Raisi wa aina gani wewe usoweza kutoa maamuzi ya
aina yoyote,hivi kweli unamwachia Borafya anapanda kwenye kiriri
anamtukana makamo wa Raisi Muheshimiwa Seif Sharrif Hamad,je kweli huu
ni utu?
Kwa ufupi CCM mumefeli na sisi wananchi tutakwenda na nyinyi
sambamba hivi hivi mpaka kijulikane na kila ukiweka viongozi wetu ndani
basi wengine wakali zaidi ndio watakuja,watu wazima hawatishani
paka,mmekuwa kama timu mbovu ya mpira mmeanza kupiga kiatu,mmeishiwa na
sera mmeona muanze kuweka mamombo kwenye viriri watukane na watutishe na
kuanza siasa za chuki, fitina na ubaguzi,kwa taarifa yenu baina ya watu
wa Unguja na Wapemba sisi sote ni wamoja,adui tunamjua na wala
hatutorudi nyuma,tutashikamana na tutasimama madhubuti msimamo wa farasi
hakuna,mpuuzi wala kibaraka atakaetuyumbisha,tuko imara na sote
tunasema kuwa ALUTA KUNTINUWA.
Mlipofanya Mapinduzi mlisema kuwa
lengo na madhumuni ilikuwa ni kupata Zanzibar huru,Zanzibar kamili na
zanzibar yenye kujitawala na yenye kuamua mambo yake ya ndani na ya nje
wenyewe,sasa leo hizo sherehe kinasherehekewa kitu gani,miaka hamsini
baada ya mapinduzi mpaka leo hakuna nchi inayoitwa Zanzibar,hakuna
bendera ya Zanzibar,raisi wa Zanzibar hajulikani akivuka chumbe,hakuna
kiti katika umoja wa Mataifa chenye jina la Zanzibar sasa izo sherehe za
uhuru za kitu gani?kipi khasa kinachosheherekewa?Zanzibar mpaka raisi
wetu akachaguliwe Dodoma,ati mbunge wa Dodoma na Sumbawanga ndio
anatuchagulia raisi wetu kwenye halmashauri kuu Dodoma,halafu mpika
gongo anatwambia miaka hamsini imeleta mafanikio,mafanikio gani?
TUNASEMAJE?ZANZIBAR KWANZA UPUUZI BAADAE
WAZEMBE KAENI PEMBENI MUWAPISHE WALOSOMA,WALOFAHAMU NA WENYE UZALENDO.
SOURCE: VOICE OF ZANZIBAR
Hatujui mnara huu utagharimu kiasi gani lakini tunajua kuwa utagharimu mamilioni ya shilingi ambazo serikali haina,lakini kwa vile wazee wa CCM wameona ni kitu ambacho ni muhimu sana basi lazima kifanyike,ijapokuwa kuna mengi ambayo yangeweza kufanywa kwa kutumia pesa hizi lakini kwa sasa kwa mjibu wa SMZ mnara ndio jambo muhimu kuliko yote.
Kwa sasa hivi mnara ni muhimu kuliko matibabu,wengi wenu mna jamaa au mmetembelea marafiki au baadhi yenu nyie wenyewe mmewahi kwenda kujaribu kupata huduma za afya katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na hali mmeiyona,kwa ufupi hali inasikitisha,hakuna cheti wala dawa,kitanda kimoja wanalala baina ya wagonjwa wawili mpaka watatu,na ukienda kwenye hio wodi ya wazazi ndio hakusemeki,hivi juzi hapa tumemzika mwanamke kijana mbichi hafiki hata miaka 40,Allah amlaze mahali pema na amsameh makosa yake,sisi tunafahamu kuwa kila mwanadamu anakufa kwa ahadi lakini lazima kuwe kuna sababu na sababu ya ndugu yetu aliefariki juzi mtoto wa Malindi bila ya shaka ulikuwa ni uzembe tena uzembe wa hali ya juu,marehemu alitokwa na damu mpaka akafariki wakati madaktari,ndugu,jamaa na wazazi wakikaa wanamuangalia bila ya kuweza kusaidia,ati imefikia kiwango kuwa daktari anasema mie siwezi kufanya kitu kwa sababu sina nyenzo za kufanyia kazi,sina gloves wala sina vifaa vya upasuaji,kwa hio ilobakia mgonjwa jifie halafu tuseme Allah ndio kaandika,hii ndio hali yetu ya mnazi mmoja,na lini umewahi kumuona muheshimiwa wa serikali akaumwa akaenda kutibiwa mnazi mmoja?
Tuende kwenye shughuli za elimu,hamuwezi kutudanganya na mtasema mnachotaka lakini takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha elimu kinazidi kuanguka siku hadi siku,kuna mashule chungu nzima ambayo yamefunguliwa ya private ambayo hayana maana yoyote,shule za serikali na za private zote ni sawa huwezi kutafautisha baina yao,zote watoto wanafeli na hakuna anaejali,na nani atakaethamini elimu ikiwa viongozi wa chama cha tawala CCM msemaji mkuu Borafya?mtu alokulia kupiga ngoma za kiluo na bomu pamoja na kupika tende pale mwembeshauri,leo mtu huyu kawa mkuu wa wilaya na moja kati ya watukanaji mashuhuri wa chama cha CCM.
Sisi ni watu wenye heshima zetu na siku zote tunaheshimu wakubwa zetu,mpaka pale wakubwa zetu wanapoonesha kutotuheshimu sisi basi na sisi tunakuwa hatuna heshima dhidi yao,kwa maana hio basi leo tunadiriki kuwaita viongozi wetu wezi na pia wazembe wa tabia,Dr Sheni kama unasoma haya utatusamehe lakini katika viongozi wewe humo wewe ni mzembe wa tabia na mburuzwaji kama mbuzi ambae hataki kunywa maji,najua watu watasema kuwa hatuna adabu lakini mpaka siku utakayo tuonesha kwamba unatujali basi sisi kwetu heshima itakuwa sio muhimu,kumbuka kuwa heshima ni kitu cha bure hatuna haja ya kununua.
Kumbuka kuwa hatujasahau maafa ya MV SPICES wala MV SKAIG,mamia ya watu waliokufa kwa uzembe na hakuna hata mzembe mmoja mpaka leo alokwenda ndani kubwa ulolifanya muheshimiwa Raisi umeona umuondoshe Mustafa Jumbe bandarini na kumpeleka kwenye idara nyengine kwa jinsi akili zenu zilivyojaa ukoko na ukosefu wa uzalendo,na kwa jinsi mlivyokuwa hamna haya wala hamjui vibaya mmekula mpaka pesa za mchango wa maafa hayo mpaka leo mayatima hawajalipwa halafu mtu kama wewe pamoja na Sefu Iddi mna uso wa kusimama mbele yetu na kusema nchi ina maendeleo?
Mmekuwa kama hamjasoma hivi kweli mmeona nyie ni bora kwenda kujenga mnara wa upuuzi wakati hata maji hayatoki majumbani,watu wamefanya vibyongo kwa kuchota maji,juzi hapa kuna mzee mmoja wa CCM alituambia maendeleo yapo kwa sababu sasa hivi baada ya watu kubeba masusu vichwani na kuuza samaki sasa hivi wanatumia baskeli na vipikipiki,maendeleo hayapimwi kwa vitu kama hivi,maendeleo yanapimwa kwa kipato,ajira,afya elimu na mambo mengine.
Ingelikuwa bora mara elfu kumi kama mngetumia pesa mkaenda kununua viti vya mashule au vitanda na madawa hospitalini,lakini hamna haya wezi wakubwa uwanja wa ndege umekushindeni pesa mmekula na sasa hivi hamjui la kufanya,nchi mmeifisidi,na mtu akisema kweli mnamuweka ndani au mnamwagia tindi kali mlivyokuwa madhalimu,mji unanuka,watu wanajijengea ovyo,majumba ya michenzani makaro yanafoka,mataka kila chochoro lakini bado mna pesa za kujengea mnara wa ujinga,sijui tuseme kwamba hamyaoni haya?Au basi mmekuwa mambumbu na vyeo vimekufanyeni muyasahau yote haya?
Mashekhe wetu mmewaweka ndani kisa ati wanahatarisha usalama,kwa taarifa yenu mashekhe wetu hawajauwa mtu,wauwaji ni nyie mlouwa watu kwenye meli zilizozama,na kweli hasa kama wewe Sheni mpenda haki mbona hujaenda kukamata machangu doa kule bwawani usiku?Au wale sio majanga kwa taifa?Tuna uhakika wale wanasambaza ukimwi je kati ya wale na mashekhe nani hatari kwa taifa?Au umeamua kuyafumbia macho kwa sababu watu walokuweka unawaogopa?Raisi wa aina gani wewe usoweza kutoa maamuzi ya aina yoyote,hivi kweli unamwachia Borafya anapanda kwenye kiriri anamtukana makamo wa Raisi Muheshimiwa Seif Sharrif Hamad,je kweli huu ni utu?
Kwa ufupi CCM mumefeli na sisi wananchi tutakwenda na nyinyi sambamba hivi hivi mpaka kijulikane na kila ukiweka viongozi wetu ndani basi wengine wakali zaidi ndio watakuja,watu wazima hawatishani paka,mmekuwa kama timu mbovu ya mpira mmeanza kupiga kiatu,mmeishiwa na sera mmeona muanze kuweka mamombo kwenye viriri watukane na watutishe na kuanza siasa za chuki, fitina na ubaguzi,kwa taarifa yenu baina ya watu wa Unguja na Wapemba sisi sote ni wamoja,adui tunamjua na wala hatutorudi nyuma,tutashikamana na tutasimama madhubuti msimamo wa farasi hakuna,mpuuzi wala kibaraka atakaetuyumbisha,tuko imara na sote tunasema kuwa ALUTA KUNTINUWA.
Mlipofanya Mapinduzi mlisema kuwa lengo na madhumuni ilikuwa ni kupata Zanzibar huru,Zanzibar kamili na zanzibar yenye kujitawala na yenye kuamua mambo yake ya ndani na ya nje wenyewe,sasa leo hizo sherehe kinasherehekewa kitu gani,miaka hamsini baada ya mapinduzi mpaka leo hakuna nchi inayoitwa Zanzibar,hakuna bendera ya Zanzibar,raisi wa Zanzibar hajulikani akivuka chumbe,hakuna kiti katika umoja wa Mataifa chenye jina la Zanzibar sasa izo sherehe za uhuru za kitu gani?kipi khasa kinachosheherekewa?Zanzibar mpaka raisi wetu akachaguliwe Dodoma,ati mbunge wa Dodoma na Sumbawanga ndio anatuchagulia raisi wetu kwenye halmashauri kuu Dodoma,halafu mpika gongo anatwambia miaka hamsini imeleta mafanikio,mafanikio gani?
TUNASEMAJE?ZANZIBAR KWANZA UPUUZI BAADAE
WAZEMBE KAENI PEMBENI MUWAPISHE WALOSOMA,WALOFAHAMU NA WENYE UZALENDO.
SOURCE: VOICE OF ZANZIBAR