Friday, 1 November 2013

Wataka wakwepa kodi nchini kusakwa

Na Hadija Jumanne,Mwananchi

Posted  Ijumaa,Novemba1  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Kauli hiyo ilitolewa juzi na wanafunzi kutoka shule 36 za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani,
wakati wa ufunguzi wa mashindano yanayohusu masula ya kodi kwa sekondari yaliyoandaliwa na TRA.

Dar es Salaam. Wanafunzi wa sekondari nchini wameitaka Serikali kuongeza juhudi katika kupambana na wafanyabiashara wanaokwepa kodi.
Pia,wameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara, kwa sababu watu wengi hawajui umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyari na kupewa risiti wanaponunua bidhaa.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na wanafunzi kutoka shule 36 za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani,
wakati wa ufunguzi wa mashindano yanayohusu masula ya kodi kwa sekondari yaliyoandaliwa na TRA.
Mmoja wa wanafunzi hao kutoka Sekondari ya Mwanalugali, mkoani Pwani, Juma Joseph alisema licha ya Serikali kupambana na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi, juhudi zaidi zinahitajika.

SOURCE: MWANANCHI