Na Fidelis Butahe na Beatrice Moses, Mwananchi
Posted Ijumaa,Oktoba11 2013 saa 24:0 AM
Posted Ijumaa,Oktoba11 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Ni ile ya ongezeko la tozo kwa magari ya mizigo yaliyozidi kilo kwa asilimia tano.
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana
amefuta agizo lililotolewa na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli la
kuwataka wamiliki wa magari makubwa ya mizigo, kutozwa asilimia tano kwa
kila gari litakalozidisha uzito na kuagiza kurudiwa kwa utaratibu wa
zamani wa msamaha wa asilimia tano ya tozo hiyo.
Pinda pia ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Wizara ya
Ujenzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Wizara ya Viwanda na
Biashara, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Uchukuzi na Ofisi ya
Waziri Mkuu kukutana na Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa),Chama cha
Wamiliki wa
Malori (Tatoa) ili kukubaliana kwa pamoja kuhusu
tozo hiyo. Agizo hilo la Magufuli alilolitoa takribani siku nne
zilizopita, liliathiri kasi ya upakuaji wa mizigo katika bandari ya Dar
es Salaam kutokana na mgomo huo wa malori.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Pinda
alisema, katika mazingira yaliyopo sasa, ushirikiano kati ya Serikali na
wadau unahitajika. “Ni lazima wadau washirikishwe ili kusiwe na
malalamiko na mambo yaende vizuri,” alishauri Pinda.
Alisema, awali utaratibu uliokuwa unatumika
ulipewa baraka na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu (sasa Ujenzi), Basil
Mramba ambaye baada ya wadau wa usafirishaji kulalamika kuhusu ubovu wa
barabara na mizani, alitoa unafuu wa kupunguza asilimia tano ya uzito
utakaosomwa katika mizani (utakaozidi).
“Lengo lake ilikuwa ni kufidia matatizo ya
upungufu wa mizani kutoweza kupima kwa usahihi uzito wa magari
yanayopimwa katika vituo mbalimbali vya mizani nchini, lakini hivi sasa
mizani yetu ni mizuri na ya kisasa,” alisema na kuongeza:
“Lakini ikumbukwe kuwa agizo hilo lilikuwa kinyume
na Sheria ya Usalama Barabarani sura ya 168 toleo la 2002 na kanuni
zake za mwaka 2001, ambayo inazuia malori kuzidisha uzito. Mramba
aliamua vile ili kumaliza hali iliyokuwa imejitokeza wakati akiwa Wizara
ya Miundombinu,”
aliongeza Pinda. Alisema kati ya kanuni hizo, kanuni ya 7(3) inatoa sharti la kama lori likibainika kuzidisha mzigo,sharti ni ama kupanga upya mzigo ili kupunguza uzito,kuushusha mzigo uliozidi au kupigwa faini mara nne ya faini ya kawaida. Pinda alisema baada ya kuibuka kwa mgomo huo alikutana na wadau wa usafirishaji na mawaziri wa wizara zenye dhamana na ujenzi na usafirishaji, kubaini kuwa kulikuwa na ulazima wa wizara hizo kukutana na wadau ili wakubaliane.
aliongeza Pinda. Alisema kati ya kanuni hizo, kanuni ya 7(3) inatoa sharti la kama lori likibainika kuzidisha mzigo,sharti ni ama kupanga upya mzigo ili kupunguza uzito,kuushusha mzigo uliozidi au kupigwa faini mara nne ya faini ya kawaida. Pinda alisema baada ya kuibuka kwa mgomo huo alikutana na wadau wa usafirishaji na mawaziri wa wizara zenye dhamana na ujenzi na usafirishaji, kubaini kuwa kulikuwa na ulazima wa wizara hizo kukutana na wadau ili wakubaliane.
Bandari walia na mgomo
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA),imeeleza
kuwa wananchi ndiyo wataumia kwa kulazimika kulipa hasara iliyotokana na
mgomo huo.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa Bandari hiyo, Janeth
Ruzangi alisema hali hiyo itatokana na wafanyabiashara kulazimika
kupandisha bei ya bidhaa mbalimbali zilizokwama kwa siku kadhaa
bandarini hapo ili kufidia gharama walizotozwa na wamiliki wa meli.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI