Friday, 11 October 2013

"KAMA NINGEKUANA UHURU WA KUTEMBEA BILA VING'ORA NINGEFANYA HIVYO"...RAISI KIKWETE AFUNGUKA!!! SOMA ZAIDI HAPA


 
 
Rais Kikwete amenukuliwa na RADIO WAPO akisema kuwa kama angekua na Uhuru wa kutembea bila Ving’ora angefanya ziara za kushtukiza kwa Wakuu wa Wilaya(DCs) na Wakuu wa Mikoa(RCs) kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uzembe.Amedai

Kauli hii ya Rais imekosa viwango vya Urais na weledi wa Amiri Jeshi Mkuu wa Ulinzi na Usalama.Ni kauli isiyokua na umaarufu wala umakini wowote.Kauli hii yenyewe ni Taswira ya uzembe na kushindwa kwa Taasisi ya Urais.Kwa Nchi zinazojali heshima ya mamamlaka ya Urais ingebidi Rais ashinikizwe ashinikizwe kujiuzulu
Rais anakiri kuwa nchi imemshinda,mamlaka ya Urais hayapo kitaasisi tena.Rais anakiri kuwa Usalama wa Taifa (TISS) hauwezi kufanya kazi hadi Rais afanye kazi za kuvizia

Tumezoea kushuhudia mtindo huu wa kuvizia ukifanywa na matrafiki barabarani,wanajificha vichakani na kujitokeza ghafla magari yanapokaribia mahali walipojificha.Mtindo huu umeingia Ikulu

Tumegeuka kuwa taiafa la kuvizia.Hivi Rais atavizia na kushtukiza idara ngapi?Watu wazima na wasomi hadi wasukumwe?Hakuna working policy?Semina Elekezi hazikufanya kazi? Je,Majina aliyokiri kuwa nayo ya wauaza madawa ya Kulevya alishindwa kuchukua hatua kwa sababu ya ving’ora?

Kumbe Ving’ora ndiyo kikwazo kwa Rais kuwacukulia hatua wezi wa EPA? Siku hizi Matamshi ya mkuu wa Nchi yanazidi kutia mashaka sana.Kauli zake ni tata.
Leo amevilaumu Ving’ora kwamba vinamzuia kufanya ziara za kufamania.Haamini tena katika mfumo imara wa kiutendaji bali weledi wa kufanya fumanizi.Ndiyo Tunajenga taifa kubwa namna hii?
 
SOURCE: PAPARAZI BLOG