Na Patricia Kimelemeta, Mwananchi
Posted Jumanne,Oktoba1 2013 saa 24:0 AM
Posted Jumanne,Oktoba1 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Dar es Salaam. Chuo Cha Mafunzo
ya Ufundi (Veta) ni miongoni mwa taasisi za elimu za Serikali
zinazoongoza kughushi vyeti kwa wanafunzi wanaoomba kazi kupitia Ofisi
ya Rais, Sekretarieti ya Ajira kwa Watumishi wa Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Sekretarieti hiyo,
Kasim Nyaki alisema kuwa, watu 517 waliotumia vyeti vya Veta kuomba
ajira kupitia sekretarieti hiyo, watu 304 walitoa vyeti halali, lakini
watu 213 walighushi.
“Baadhi ya watu walioomba ajira kupitia
sekretarieti yetu ambao wamebainika kutumia vyeti vya Veta ambavyo
vimeghushiwa, jambo ambalo limeonyesha wazi kuwa, taasisi hiyo ya elimu
inaongoza kwa watu kughushi vyeti vyao,”alisema Nyaki.
Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, zaidi ya
watu 13,554 walioomba ajira katika kipindi cha miaka mitatu, watu 816
wamebainika kughushi kwa kutumia vyeti vya taasisi mbalimbali iwe ya
elimu, vyeti vya kuzaliwa na vinginevyo.
Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, wananchi
wanapaswa kuacha tabia ya kughushi vyeti hivyo kwa sababu vinaweza
kuwaletea matatizo katika maisha yao.
Hata hivyo, Nyaki alisema kuwa, wanafunzi
wanapaswa kusoma masomo ya sayansi ili waweze kupata uhakika wa ajira
kwa sababu nafasi nyingi zinazotokana na masomo hayo.
Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, wanapaswa
kujijengea utaratibu wa kupenda kusoma masomo hayo ili waweze kupata
uhakika katika soko la ajira, jambo ambalo linaweza kupunguza matatizo
ya upatikanaji wa ajira za Serikali.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI