Posted Jumanne,Oktoba1 2013 saa 13:21 PM
Kwa ufupi
Taarifa ya uamuzi huo imetolewa leo kwenye mkutano
wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, ikiwa ni hatua mihimu ya
kuthibitisha tangazo lake la Julai mwaka huu kwamba atawapa heshima
viongozi hao wawili wa juu wa Kanisa waliopita katika karne ya 20.
Vatican. Papa John Paul II na John XXIII
wanatarajiwa kutangazwa watakatifu Aprili 27 mwakani, kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na mkuu wa sasa wa kanisa Katoliki, Papa Francis.
Taarifa ya uamuzi huo imetolewa leo kwenye mkutano
wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, ikiwa ni hatua mihimu ya
kuthibitisha tangazo lake la Julai mwaka huu kwamba atawapa heshima
viongozi hao wawili wa juu wa Kanisa waliopita katika karne ya 20.
Katika taarifa iliyonakiliwa kutoka kwenye gazeti
la mtandaoni la Daily Mail, alisema wakuu hao wa Kanisa Katoliki duniani
ambao kwa sasa ni marehemu waliweza kutumia karama zao kwa uamunifu na
kuonyesha matendo makuu.
Wachambuzi wa masuala ya Kanisa hilo alieleza
kwamba inaonekana umuzi huo ni wa makusudi ikiwa ni hatua ya kujaribu
kuliunganisha kanisa hilo ambalo lina mkanganyiko kwa sasa.
Kila mmoja ana watu wanaomuunga mkono na
wanaompinga, ambapo kwa sasa Francis anaonekana kuungwa mkono na wote wa
pande zote mbili hivyo kuwa kichocheo cha kuunganisha na kufuta makovu
yaliyolikumba Kanisa hilo kwa miaka ya hivi karibuni.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI