Friday, 18 October 2013

Waonywa kulinda waasi

Na Robert Kakwesi

Posted  Ijumaa,Oktoba18  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Akizungumza kwenye mkutano wa waumini wa Kikristo na Kiislamu wa kuombea amani ya nchi,Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa,alisema wengi wa raia hao hawajui asili ya nchi zao bali Tanzania na baada ya kupata uraia wasijihusishe na kuvuruga amani kwa madai ya kujihusisha na vikundi vya uasi vya nchi jirani .

Kaliua. Watanzania wenye asili ya Burundi na Kongo,waliopo katika makazi ya Ulyankulu, wilayani hapa,wameonywa kutojihusisha na vikundi vya uasi na nchi jirani kwani kuwa wao sasa ni Watanzania halisi.
Akizungumza kwenye mkutano wa waumini wa Kikristo na Kiislamu wa kuombea amani ya nchi,Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa,alisema wengi wa raia hao hawajui asili ya nchi zao bali Tanzania na baada ya kupata uraia wasijihusishe na kuvuruga amani kwa madai ya kujihusisha na vikundi vya uasi vya nchi jirani .
“Nyinyi sasa mjielewe ni Watanzania na hakuna sababu ya kujihusisha na vikundi vya uasi vya nchi jirani na ninapenda mjisikie ni Watanzania,”aliwaleza na kushangiliwa.
Alisema kama wameomba na kupewa uraia wao ni Watanzania na kuwataka wajisikie hivyo na kutoa taarifa za wale wote wanaokwenda kinyume cha sheria za nchi.
Hivi karibuni kumeripotiwa kuwapo na uvamizi unaodaiwa kufanywa na wageni.

SOURCE: MWANANCHI