Friday, 1 November 2013

Mbaroni kwa kuuza ‘chupi’ za mitumba


Na Beatrice Moses,Mwananchi

Posted  Ijumaa,Novemba1  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Operesheni hiyo iliyohusisha polisi, iliwafanya wafanyabiashara wengi wa nguo hizo kutimua mbio na kutelekeza bidhaa hizo.


Dar es Salaam. Watu watatu wamekamatwa baada ya kukutwa wakiuza nguo za ndani na soksi kinyume cha sheria, hivyo kuhatarisha afya za wananchi.
Watu hao ambao majina yao yanahifadhiwa walikamatwa jana wilayani Temeke,Dar es Salaam katika operesheni inayofanywa na Shirika la Viwango Nchini (TBS) linalolenga kuondoa nguo za aina hiyo kwenye masoko ya mitumba nchini.
Operesheni hiyo iliyohusisha polisi, iliwafanya wafanyabiashara wengi wa nguo hizo kutimua mbio na kutelekeza bidhaa hizo.
Ofisa Afya wa Manispaa, Leonard Chigalula alisema,watu hao watashtakiwa katika mahakama za manispaa zinazosimamia masuala ya afya kwa kuwa nguo hizo zinahatarisha afya za wananchi kwa kupata maambukizi ya magonjwa ikiwamo fangasi. Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile alisisitiza kuwa operesheni hiyo ni endelevu na kuwasihi wafanyabiashara hao kutafuta biashara nyingine.

SOURCE: MWANANCHI