Na Tausi Ally, Mwananchi
Posted Alhamisi,Oktoba24 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Oktoba24 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Kabla ya madai hayo, Hakimu Mkazi, Hellen Liwa aliuuliza upande wa mashtaka kuhusu ulipofikia upelelezi wa kesi hiyo.
Dar es Salaam. Mshtakiwa Makongoro Joseph
Nyerere, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, amelalamika kuwa amebambikiziwa
kesi hiyo.
Alidai kitendo hicho kilikuja baada ya kukataa kutoa rushwa ya Sh 8 milioni polisi.
Madai hayo aliyatoa jana mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Liwa, wakati kesi hiyo ilipofikishwa kwa kutajwa.
Makongoro na mfanyabiashara maarufu jijini Dar es
Salaam, Abubakar Marijan (50), maarufu Papaa Msofe wanashtakiwa kwa
tuhuma za kumuua mfanyabiashara wa madini, Onesphory Kituli mwaka 2011.
Kabla ya madai hayo, Hakimu Mkazi, Hellen Liwa aliuuliza upande wa mashtaka kuhusu ulipofikia upelelezi wa kesi hiyo.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado unaendelea na baada ya maelezo hayo, mshtakiwa Makongoro alianza kulalamika.
“Mheshimiwa mimi kesi hii nimebambikiwa baada ya
kukataa kutoa rushwa ya Sh8 milioni, naomba mahakama itumie mamlaka yake
kuona haki inatendeka,” alilalamika Makongoro.
Alidai kuwa upande wa mashtaka umekuwa ukitoa taarifa zinazokinzana kuhusu upelelezi.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI