Na Shaban Lupimo, Mwananchi.
Posted Alhamisi,Oktoba24 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Oktoba24 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Hatua hiyo inafuatia malalamiko yaliyotolewa na wakulima wa mahindi katika Mkoa wa Njombe.
Njombe. Rais Jakaya Kikwete, amemwagiza Mkuu wa
Mkoa wa Njombe, Aseri Msangi na watendaji wake, kuangalia namna ya
kuruhusu sekta binafsi kununua tani 2,672,902 za mahindi kutoka kwa
wakulima Ludewa.
Pia ametaka wakulima hao waruhusiwe kuuza mahindi yao nje ya nchi.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana alipokuwa
akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Njombe, katika majumuisho ya ziara
yake katika mkoa huo mpya.
“Kuwazuia wakulima kuuza mahindi yao nje ya nchi ni kuwatajirisha wanaokaa kwenye vizuizi na kufanya ulanguzi.
“Ni lazima mkoa uhakikishe kuwa wakulima
wanawekewa utaratibu mzuri ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu kuuza mazao yao
nje ya nchi,” alisema Rais.
Alisema kufanya hivyo, kutatoa nafasi kwa wakulima, kuinua vipato vyao.
Alisema hatua hiyo inapaswa kwenda sambamba na ya
kuiruhusu sekta binafsi kununua mahindi yaliyopo ili kuondoa uwezekano
wa kuwanufaisha wachache.
“Maghala yetu ya akiba ya chakula yana uwezo wa
kubeba tani 250,000 kwa hiyo kwa sasa tunatoa fursa kwa sekta binafsi
nao watusaidie katika hili maana sisi Serikali tumejaza maghala yetu,”
alisema.
Pia aliwataka viongozi kuendelea kuwahimiza wananchi kulima mazao ya biashara, hasa miti, kahawa, mbogamboga na matunda.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI