Na Peter Saramba na Elias Msuya, Mwananchi
(email the author)
Posted Alhamisi,Juni20 2013 saa 21:15 PM
Posted Alhamisi,Juni20 2013 saa 21:15 PM
Kwa ufupi
kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha vifo
pamoja na zile zilizofuatia wakati polisi ilipowasambaratisha wafuasi wa
chama hicho kwa mabomu walipokusanyika kwenye Viwanja vya Soweto kwa
lengo la kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Wakiongozwa na mawakili watatu, Mbowe na Lema waliwasili polisi saa 3.50 asubuhi na kuhojiwa hadi saa 9.10.
Viongozi hao walipokewa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa
wa Arusha, Diwani Nyanda kabla ya kutenganishwa kwenye vyumba viwili
tofauti kwa mahojiano.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mbowe, Lema na
wakili Albert Msando walitaja mambo mawili ambayo polisi waliwahoji
kwanza ikiwa ni ushiriki wao katika mkusanyiko usio halali kwenye
Viwanja vya Soweto, Jumanne iliyopita ambao ulisambaratishwa na polisi.
Jambo jingine ambalo polisi iliwahoji ni kauli yao
ya kuwa na ushahidi unaohusisha polisi na tukio la bomu lililorushwa
kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha vifo vya watu wanne huku zaidi
ya 60 wakijeruhiwa.
Mbowe alisema kwa pamoja wamewaeleza polisi kuwa
hawaamini kama mkusanyiko wa Jumanne iliyopita haukuwa halali kwa sababu
waliruhusiwa kuzungumza na wananchi waliokusanyika ili kuwashawishi
watawanyike.
“Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) wa Arusha, Gilles
Mroto ndiye aliyeturuhusu kuzungumza na wananchi wale kuwataka
watawanyike na ndicho tulichofanya, lakini tukashangaa kuanza kupigwa
mabomu mara baada ya kuwataka watu wanaotaka kutoa heshima za mwisho kwa
marehemu kwenda Hospitali ya Mount Meru,” alisema Mbowe.
Alisema Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna
Paul Chagonja kuwa naye aliyewaomba viongozi wa Chadema kuwatawanya
wafuasi wa chama hicho baada ya kuzuiwa kutoa heshima za mwisho katika
viwanja hivyo vinavyomilikiwa na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha
(AICC).
Msimamo wa Mbowe
Kuhusu ushahidi anaodai unawahusisha polisi na
tukio la bomu, Mbowe alisisitiza kuwa Chadema kina ushahidi wa kutosha
kuthibitisha hilo lakini alisema hakitaukabidhi mikononi mwa polisi.
Alisema hakitafanya hivyo kwa kuwa jeshi hilo ni
watuhumiwa wakuu hivyo hawawezi kuwa na dhamira na nia njema katika
upelelezi wao. Alisema ndiyo maana badala polisi kuwaona ni msaada,
kimeanza kutoa vitisho kwa wote wanaosema waliwashuhudia askari
wakishambulia watu kwa risasi kabla ya kuondoka na aliyerusha bomu
kwenye gari lao.
“Chadema tuko tayari kukabidhi ushahidi huu kwa
tume huru ya uchunguzi ya Mahakama. Rais Kikwete atumie mamlaka yake ya
kikatiba kuunda tume kuchunguza tukio la bomu Arusha ili ukweli
ujulikane. Polisi ni watuhumiwa katika jambo hili, hivyo hawana dhamira
safi na ushahidi wetu,” alisema Mbowe.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi inawasiliana na wanasheria
kutafuta ushauri wa hatua za kuchukua... “Polisi ndiyo wenye jukumu la
kuchunguza na kukusanya ushahidi wote kuhusiana na matukio ya uhalifu.
Hili ni jukumu la kisheria la polisi. Chadema wakabidhi ushahidi wao
badala ya kupiga danadana ya kutaka tume huru ya uchunguzi ya
kimahakama.”
Alisema hata ikiundwa tume, bado jukumu la
kuchunguza na kukusanya ushahidi litarejeshwa mikononi mwa polisi, hivyo
Chadema wanapaswa kutimiza wajibu wa kusaidia uchunguzi kwa kuwasilisha
ushahidi wao wa polisi kuhusika katika tukio la bomu.
Askofu alia na dola
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Jimbo la Arusha Mashariki, Isaac Kisir ameitaka Serikali
kuchukua hatua kali kulinda usalama huku akivitaka vyombo vya ulinzi na
usalama kujitathmini kiutendaji.
Akizungumza katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa
kada wa Chadema, Judith Moshi iliyofanyika katika Usharika wa Sokoni
One, Askofu Kisir alisema mlipuko wa bomu haukuwa mapenzi ya Mungu, bali
ni ugaidi.
“Tunapomzika mwenzetu lazima tuseme ukweli,
tusimung’unye maneno, ukweli utatuweka huru. Nchi yetu sasa haina
usalama ule tuliokuwa nao. Kumekuwa na utekaji nyara watu wanaosema
ukweli. Kumekuwa na matumizi ya nguvu kupita kiasi kwa vyombo vya
usalama, uchomaji wa makanisa na milipuko ya mabomu.
“Tulitegemea Serikali itatoa adhabu kwa
wanaohusika lakini tunasikia maneno ya kejeli… mara tuko mbioni, mara
tuko imara, huku watu wanauawa na kupata vilema.”
Judith ni mmoja wa watu wanne waliouawa katika
shambulio la bomu lililolipuka wakati wa kuhitimisha kampeni za udiwani
za Chadema katika Viwanja wa Soweto Juni 15 mwaka huu, huku watu wengine
zaidi ya 60 wakijeruhiwa.