Kwa ufupi
Arusha. Mwanasiasa mkongwe
nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki
za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka
demokrasia inapozuia wagombea binafsi.
Katika hukumu iliyosomwa leo jioni, mahakama
imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa,
Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye
uongozi.
Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya
kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri
mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua
mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye
mahakama za kitaifa.