Kwa ufupi
- Mkurugenzi wa NEC,Julius Malaba alisema jana Dar es Salaam kuwa kutokana na hali hiyo, wananchi wa eneo hilo wanapaswa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura,ili waweze kuhakiki majina yao ili kuondoa usumbufu siku ya kupiga kura.Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo wananchi wa eneo hilo wametakiwa kutulia kwenye makazi yao mpaka uchaguzi utakapofanyika tena.
Dar es Salaam.Tume ya Uchaguzi (NEC) imetangaza
kurudiwa kwa uchaguzi mdogo katika kata nne za Arusha ambazo ni
Kimandolu, Elerai, Themi na Kaloleni ambazo zilisimamishwa kufanyika kwa
uchaguzi mdogo wa madiwani kutokana na vurugu zilizojitokeza katika
kampeni za mwisho za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na sasa
utafanyika Juni 30 mwaka huu.
Mkurugenzi wa NEC,Julius Malaba alisema jana Dar
es Salaam kuwa kutokana na hali hiyo, wananchi wa eneo hilo wanapaswa
kwenda kwenye vituo vya kupigia kura,ili waweze kuhakiki majina yao ili
kuondoa usumbufu siku ya kupiga kura.Aliongeza kuwa kutokana na hali
hiyo wananchi wa eneo hilo wametakiwa kutulia kwenye makazi yao mpaka
uchaguzi utakapofanyika tena.
Malaba alisema ikiwa NEC imetangaza kusimamisha
uchaguzi katika maeneo yoyote nchini, wanasiasa wanapaswa kuacha kufanya
kampeni mpaka uchaguzi utakaporudiwa tena, na kwamba ikiwa baadhi ya
vyama vitabainika kwenda kinyume na sheria hiyo vitafikishwa kwenye
kamati ya maadili kwa sababu watakuwa wamevunja sheria za uchaguzi.
Alisema, kutokana na hali hiyo,wananchi wanapaswa
kuwa makini katika kipindi hiki na kuhakikisha kuwa hawashiriki kwenye
mikutano ya kampeni inayofanyika maeneo yao ili kuondoa migogoro ambayo
inaweza kujitokeza.