HABARI ZA SASA KWA UFUPI
Wabunge wa Chadema, Mh Lema, Mh John Mnyika, Mh Mashishanga, Mh Tundu Lissu na Grace Kiwhelu wakiwa wamebeba jenenza leneye mwili wa marehemu Judith William Moshi kuelekea makaburi ya Sokoni 1 kwa maziko. Marehemu Judith alifikwa na mauti baada ya kulipukiwa na bomu siku ya Mkutano wa Chadema kuhitimisha kampeni zake kwa udiwani wa Kata ya Kaloleni, mkutano uliofanyika uwanja wa Soweto siku ya Jumamosi Juni 15, 2013. Wabunge wengi wa Chadema walishiriki ibada na kuhudhuria mazishi wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Freeman Mbowe.
Msafara wa wafuasi wa Chadema ukitoka Hospitali ya Mt Meru kuelekea Kata ya Sokoni 1 ambako ndipo misa ya kumuombea marehemu na maziko ya Judith Moshi aliyekufa kwakulipuliwa na bomu Jumamosi iliyopita ilifanyika
Msafara ukikatiaza mitaa ya Jiji kiasi cha kusimamisha shughuli zote katika njia ilikopitia


Hapa ni Sugu akiwa na Peter Msigwa wakiongoza msafara.

Hili ndilo jeneza lililolobeba mwili wa marehemu ukipelekwa Sokon 1
Vijana walioko kwenye mafunzo ya upolisi wakiwa juu ya kanisa linaloendelea kujengwa wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Judith William Moshi. Chadema inawatuhumu Polisi ndio waliolipua bomu na kupiga risasi zilizoua 4 na kujeruhi zaidi ya 67 katika mkutano wake