Tuesday 11 June 2013

Hatimaye Mkurugenzi wa usalama na ulinzi Nd. W. Lwakatare CHADEMA kupata dhamana leo

Hatimaye Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Muganyizi Lwakatare leo atapata dhamana na kurudi uraiani, baada ya Mahakama ya Kisutu kuamua kuwa dhamana yake iko wazi na sasa masharti tu ndiyo yanakamilishwa.

Mkurugenzi wa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene anadai jaribio la watawala kwa kutumia vyombo vya dola, kutaka kukichafua kwa kukipaka matope ya ugaidi na mauaji chama chao limeshindwa vibaya.
 Hatimaye Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Kamanda Wilfred Muganyizi Lwakatare 'Lwaks' leo atapata dhamana na kurudi uraiani, baada ya Mahakama ya Kisutu kuamua kuwa dhamana yake iko wazi na sasa masharti tu ndiyo yanakamilishwa.

Lwakatare anapata dhamana, huku jaribio la watawala kwa kutumia vyombo vya dola, kutaka kukichafua kwa kukipaka matope ya ugaidi na mauaji CHADEMA likiwa limeshindwa vibaya.

It's has been a battle, very seriuos battle, legally and politically, of almost three months. Bungeni, kwenye majukwaa ya siasa na mahakamani. Fighting for justice, hopes and dignity of being.

And the battle still goes on. Aluta continua.

Mapambano yataendelea kwa sababu sasa tunaanza kuamini kuwa akina Hitler, Botha na wengine wa namna hiyo bado wanaishi kwa namna nyingine, kupitia baadhi ya watu waliokabidhiwa madaraka ya kuongoza lakini wameamua kutawala.

Usikubali kufumbia macho uonevu wowote, mahali popote, kwa mtu yeyote. Ukikaa kimya leo, akina Hitler wetu hawa wa zamu zetu, watakapokufikia wakati wa 'zamu' yako hakutakuwa na mtu wa kukusemea.

Ni muhimu makamanda wasimame kwenye haki, utu, upendo, kweli na matumaini kwa ajili ya Watanzania hawa wanyonge. Mengine yote yatafuata.

Asanteni kwa kuonesha nguvu ya umma (people's power) kwa kufuatilia suala hili tangu siku ya kwanza na hadi litakapofika mwisho kwa namna nyingine linavyoendelea sasa mahakamani.

Tunaanza Mungu, tunaendelea Mungu, tutamaliza na Mungu...
 Makene.
 
Imenukuliwaa kutoka: www.jamiiforum.com