Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia, jana aliingia matatani baada ya kutakiwa kutoa maelezo ya kauli yake kuwa vitabu vilivyopo nchini ni sumu kwa Taifa.
Agizo hilo lilitolewa na Spika wa Bunge, Anne
Makinda ambaye alisema kuwa maneno yaliyotolewa na Mbatia ni mazito na
kama hayatatolewa ufafanuzi yanaweza kuleta madhara makubwa.
Mbatia alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la
nyongeza kufuatia swali lake na msingi ambalo alitaka kujua vitabu vya
hisabati kwa shule za sekondari, ambavyo havikuandikwa kwa ubora
unaokubalika.
Mbunge huyo pia alihoji wataalamu ambao walipewa
kazi ya kupitia vitabu hivyo hawakuweza kubaini udhaifu huo na kama
waliuona licha ya kuwa walitumia zaidi ya Sh24.4 bilioni huku Wizara
ikidanganya kuwa vitabu hivyo, vilipewa ithibati mwaka 2011 wakati
ithibati ilitolewa Oktoba 2010.
“Huu ni uongo tena uongozi mbaya, na ninataka
Waziri atuambie hawa waliotoa majibu ya uongo wanachukulia hatua gani
pamoja na kutumia Sh24 bilioni, kwa nini wasifukuzwe kazi, hii ni sumu
kali kwa Taifa,” alihoji Mbatia.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip
Mulugo alisema kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilikubaliana
na Chuo Kikuu Cha Jimbo la Carolina na Shirika la Usaid kutumia vitabu
vilivyoandikwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar.
Alisema kuwa mpango huo ulifuatia ombi la Rais
Jakaya Kikwete la mwaka 2009 ambapo aliomba vitabu vya sayansi na
Hisabati kutoka Serikali ya Marekani.
Alikanusha kuwa hakuna sumu yoyote ambayo
wataalamu waliiweka katika mitalaa hiyo kwani waliweza kupitia vizuri na
kwamba makosa yaliyobainika hayakuwa makubwa.
- Ndugai anapokwazwa Spika kutokuwa mbunge
- TTCL, hospitali nne nchini kutoa matibabu mtandao
- Wizara kutenga bajeti ya mazingira
- DC apiga marufuku uuzaji mahindi
- Vijana washauriwa kujikita kwenye kilimo, ufugaji
- Wakulima wakubali kupokea malipo kidogo
- Wananchi wakamata mali za wezi wa fedha za mikopo
- Watakiwa wasiuze mpunga ukiwa shambani
- ‘Bandari Dar maficho ya wahalifu’
- Upinzani wajipanga kuungana 2015
- Kibanda : Sitanyamaza kwa unyama huu
- Katiba Tanzania Bara yanukia
- Spika ampandishia Mbatia kwa kutamka ‘ sumu’
- Wanasheria wapinga Rais kuteua Jaji Mkuu
- Mtei akosoa mgombea binafsi kuruhusiwa
- Undani kifo cha Ngwea
- Kumpandisha cheo Kamuhanda ni kuwakebehi Watanzania
- Ndugai apinga Spika kutokuwa mbunge
- Ngwair kuagwa leo
- Kesi dhidi ya Ruto kuhamishiwa Kenya au Tanzania