Kwa ufupi
- DPP anapoona hana mashahidi thabiti wa kuja kujenga kesi yake anatumia kifungu hicho kufuta kesi kwani kuendelea kuwa na kesi za jinai mahakamani ambazo anaona kabisa hana mashahidi thabiti wa kuwaleta mahakamani ni matumizi mabaya ya sheria na kuisababishia Serikali gharama pamoja na mrundikano wa kesi mahakamani
kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini Wakili wa
Serikali, Awamu Mbangwa aliwasilisha hati hiyo, chini ya Kifungu cha 91
(1) cha Mashauri ya Jinai (CPA), kwa niaba ya DPP akiomba kesi hiyo
ifutwe kwa sababu hana nia ya kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao.
Baada ya kuwasilisha hati hiyo, Hakimu Mugeta
alikubaliana na ombi hilo na kuifuta. Mmoja wa mawakili wanaowatetea
washtakiwa hao, Alex Mgongolwa alisema hawana pingamizi la kufutwa kwa
shauri hilo ingawa walitaka waelezwe sababu za hatua hiyo.
Mgongolwa alisema walitaka kujua sababu hizo kwani
walikuwa na wasiwasi kuwa wateja wao wangeachiwa huru na kukamatwa tena
baada ya muda mfupi na kupandishwa kizimbani.
Kutokana na shaka hiyo, waliiomba Mahakama kuwapa kinga.
Akiifuta kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 3/2013
na kuwaachia huru washtakiwa hao ambao ni Simba na wenzake, Salum
Mwaking’inda na Meneja wa Shirika hilo, Victor Milanzi, Hakimu Mugeta
alisema maombi ya upande wa mashtaka yamekubaliwa.
Akizungumzia uamuzi huo wa DPP wa kuwafutia kesi
wateja wake, nje ya viwanja vya mahakama hiyo, Wakili Mgongolwa
alipongeza uamuzi huo akisema ni matumizi ya sheria.
“DPP anapoona hana mashahidi thabiti wa kuja
kujenga kesi yake anatumia kifungu hicho kufuta kesi kwani kuendelea
kuwa na kesi za jinai mahakamani ambazo anaona kabisa hana mashahidi
thabiti wa kuwaleta mahakamani ni matumizi mabaya ya sheria na
kuisababishia Serikali gharama pamoja na mrundikano wa kesi mahakamani,”
alisema Mgongolwa.
Mapema Aprili 30, mwaka huu, upande wa mashtaka
uliifuta kesi ya awali ya matumizi mabaya ya madaraka iliyokuwa
ikimkabili Simba na wenzake wawili na kisha kuwafungulia kesi nyingine
ya mashtaka sita ya rushwa na uhujumu uchumi. Katika kesi hiyo namba 3
ya 2013, washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya matumizi
mabaya ya madaraka na kughushi. Walifikishwa kwa mara ya kwanza
mahakamani hapo Mei 29, 2012 kujibu shtaka la kulisababishia shirika
hilo hasara ya Sh8.4 bilioni.
Walidaiwa kuwa kati ya Septemba 2009 na Januari
2010, walikula njama za kutenda kosa la vitendo vya rushwa, kinyume cha
Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
Pia walidaiwa kufanya vitendo vya rushwa kati ya
Septemba 2009 na Januari 2010 kwa kukubali kupokea Sh320 milioni kama
ushawishi wa kuiuzia Simon Group hisa za Uda ambazo zilikuwa
hazijagawiwa.