PICHA: Dr. Slaa Atembelea Shirika la Umeme Marekani ni katika mfululizo wa safari yake ya kujiifnunza iitwayo vision Tanzania
Dr. Slaa anaendelea na safari yake ya kujifunza inayoitwa “Vision Tanzania”
ambayo leo imemfikisha katika kituo kikubwa cha Umeme kinachoitwa
Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua,
gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na
nuklia
Kwa upande wake, Dr. Slaa amejifunza na kugundua kitu kimoja kwamba,
watanzania wanaumia kutokana na wachache kuligeuza Tanesco kuwa mradi
wao. Dr. Slaa anaamini kwamba mgao tulionao Tanzania, ukosefu wa umeme
tulionao ni matunda ya ufisadi wa CCM. Kiongozi huyo anaamini kwamba
tatizo ni ccm na desturi yao ya kulindana.
ilahali tunatengeneza 600MW
huku Waziri Muhongo akidai mwakani tutauza umeme nje ya nchi. Umeme gani
wa kuuza nje ya nchi wakati 80% ya watanzania hawana umeme? Huyu mtu
yuko katika sayari gani? Miaka 52 ya ufisadi, kugawana vyeo kindugu,
umasikini na magonjwa sasa tuseme basi. CCM hawawezi kujidai kwamba
watatatua matatizo ya watanzania
Viongozi wakuu Wizarani na Tanesco wanawazuia na kuwadhalilisha
wawekezaji kwa manufaa yao binafsi na makampuni yasiyokuwa na huruma na
mwananchi wa kawaida. Njia pekee ya kumuokoa mtanzania, ni mtanzania
mwenyewe kuamka, na kumng’oa adui CCM kupitia njia ya kura. Mtanzania
asifanye kosa tena 2015. Lazima amn’goe CCM ili apate umeme na kuweza
kuboresha maisha yake
Akitembelea mitambo inayopewa ulinzi wa kipekee, Dr. Slaa amejionea
jinsi kampuni hiyo inavyofanya shuguli zake pamoja na kuwa na mitambo ya
kisasa inayo monita njia zote za umeme kusini mwa marekani yaani,
Georgia, Florida, Alabama, Mississini na South Carolina.
Mkurugenzi wa shirika hilo, amemuahidi Dr. Slaa kwamba wako tayari kuja
Tanzania na kuisadia nchi hiyo kuboresha uzalishaji, usambazaji pamoja
na uendeshaji ikiwa serikali itawahitaji, kwani wameisadia nchi za
Philippines na Kuwait ambazo hadi sasa wanazo umeme wa uhakika.
Dr. Slaa na ulinzi wake wakiwasili katika ofisi za Shirika la Alabama Power Company
Dr. Slaa anaelekea kwenye ofisi za shirika
Mkurugenzi mkuu akimpokea Dr. Slaa na Mkewe
Mkurugenzi wa shirika akimpa maelezo Dr. Slaa jinsi shirika hilo linavyofanya kazi
Sehemu maalum yenye ulinzi mkali ambako gridi inakuwa monitored
Dr. Slaa akitizama kwa umakini mitambo hiyo ya kusisimua inayoongoza
gridi kusini mwa marekani.Hata mashine moja ikiharibika watagundua
maramoja na kuweza kutafuta njia mbadala
Dr. Slaa akikabidhiwa kitabu na mwanasheria mkuu wa shirika hilo