Na Godfrey Kahango, Mwananchi
Posted Jumatatu,Oktoba21 2013 saa 10:17 AM
Posted Jumatatu,Oktoba21 2013 saa 10:17 AM
Kwa ufupi
Viongozi hao walisema kuwa wananchi wa jiji
hilo wamepeleka ‘pepo’ bungeni ndio maana mbunge huyo amekuwa kinara wa
vurugu ndani ya Bunge, hivyo wananchi wa Mbeya Mjini wamempeleka mtu
anayehitaji kuombewa.
Mbeya. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT), Sofia Simba na Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa waMbeya,
Dk Mary Mwanjelwa (CCM), juzi walitumia muda mwingi jukwaani
kumnangaMbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema)
wakimfananisha na `pepo’ aliyekwenda bungeni kwa ajili ya kufanya
vurugu.
Viongozi hao walisema kuwa wananchi wa jiji hilo
wamepeleka ‘pepo’ bungeni ndio maana mbunge huyo amekuwa kinara wa
vurugu ndani ya Bunge, hivyo wananchi wa Mbeya Mjini wamempeleka mtu
anayehitaji kuombewa.
Walitoa kauli hiyo juzi wakati wakihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la wazi la Kata ya Manga
Mjini Mbeya.
Simba, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, alisema hali hiyo ya ‘mapepo’ mara kadhaa imekuwa
ikimsababishia mbunge huyo kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu,
likiwemo tukio la hivi karibuni kupigana bungeni badala ya kuibua hoja
za maendeleo. Juhudi za gazeti hili za kumtafuta Sugu zilikwama jana
baada ya kuelezwa na watu wake wa karibu kuwa alikuwa safarini China.
Simba alisema tukio la mbunge huyo kupigana na
askari wa bunge ndani ya ukumbi, lilitokea kwa kuwa hakukuwa na mtu wa
kuombea ‘mapepo’ siku hiyo baada ya kumkumba ghafla mbunge huyo.
“Siku ile tukio linatokea bahati mbaya sana
Mchungaji Lwakakatare (Mbunge wa Viti Maalumu Getrud Lwakatare)
hakuwemo ukumbini maana angeweza kuyaombea na hivyo naomba wananchi wa
Mbeya msituletee ‘mapepo,” alisema.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI