5 Agosti, 2013 - Saa 12:53 GMT
Serikali ya Kenya imefutilia
mbali leseni zote za uchimbaji wa madini ambazo ilikuwa imetoa kwa
makampuni ya uchimbaji katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu.
Waziri wa madini Najib Balala, alisema kuwa
serikali iliyopita ya Rais Mwai Kibaki iliafikia mikataba kwa haraka
sana na makampuni ya uchumbaji bila ya kuzingatia uwazi katika kutoa
kandarasi za uchimbaji.Pia alimfuta kazi kamishna wa madini (Moses Masibo). Wiki jana shirika la fedha duniani IMF lilielezea wasiwasi kuhusu mikataba ambayo serikali ya Kenya ilikuwa imeafikia na makampuni ya uchimbaji likisema ilifanywa kwa usiri mkubwa.
Kenya hivi karibuni iligundua sehemu kadhaa za nchi zenye madini kama vile titanium, copper na niobium inayopsemekana kuwa na thamani ya mabilioni ya dola.
Chanzo: BBC Swahili