Monday 5 August 2013

Al-Bashir akataliwa kupita Saudi Arabia


5 Agosti, 2013 - Saa 07:23 GMT

Wakuu wa Sudan wanasema Rais Omar al-Bashir amezuwiliwa kuingia katika anga ya Saudi Arabia, na amelazimika kurudi Khartoum.
                          Rais Omar al-Bashir
Bwana al-Bashir alikuwa njiani kuelekea Iran kwa sherehe ya kutawazwa kwa rais mpya, Hassan Rouhani.
Saudi Arabia - ambayo ina uhusiano mbaya na Iran - haikutoa sababu ya kuchukua hatua hiyo.
Bwana al-Bashir anasakwa na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, kwa uhalifu wa vitani.
Mwezi uliopita al-Bashir alipewa heshima ya gwaride nchini Nigeria alipohudhuria mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika.

chanzo: BBC Swahili