Na Mwandishi Wetu 
            (
email the author)
    
Posted 
    Alhamisi,Julai18 
2013 
saa
22:46 PM
            
Kwa ufupi
Ilipangwa kujenga tanki lenye uwezo wa 
kuhifadhi maji lita 135,000, lakini mkandarasi aliamua kujenga tangi 
lenye uwezo wa kuhifadhi lita 90,000 ili kuuunganisha na tanki la zamani
 lenye uwezo huohuo lakini mkandarasi hakuunganisha matanki hayo jambo 
ambalo ni kosa’’ alisema..
 
Tanga. Katika hatua inayoashiria kuchoshwa na utekelezaji usioridhisha wa miradi, Mbunge wa 
Jimbo
 la Bumbuli, wilayani Lushoto, January Makamba amekataa kuupokea mradi 
wa maji uliojengwa katika Halmashauri Mpya ya Bumbuli kutokana na kile 
alichokieleza kuwa umejengwa chini ya kiwango.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara 
uliofanyika Bumbuli, Makamba, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na 
Teknolojia alisema kuwa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh400 
milioni haukutekelezwa ipasavyo pamoja na kutengewa fedha nyingi na 
wahisani ambao ni Benki ya Dunia.
Mradi huo umepangiwa kuwanufaisha, wanakijiji katika vijiji 
vinne vya Bumbuli Mission, Bumbuli Kaya, Mboki na Kwamanolo na ulikuwa uanze kutoa huduma ya maji kuanzia Kijiji cha Kwamanolo.
“Ilipangwa kujenga tanki lenye uwezo wa kuhifadhi 
maji lita 135,000, lakini mkandarasi aliamua kujenga tangi lenye uwezo 
wa kuhifadhi lita 90,000 ili kuuunganisha na tanki la zamani lenye uwezo
 huohuo lakini mkandarasi hakuunganisha matanki hayo jambo ambalo ni 
kosa’’ alisema..
Alisema fedha zilizotumika na thamani halisi ya 
mradi ni tofauti na kwamba ni vigumu kwake kuamini kwamba mradi huo 
utatekelezwa kama ulivyokusudiwa awali.
Alisema ni afadhali asipokee kwanza mradi huo ili 
taratibu zingine za kuchunguza zifanyike kama ni kweli mradi huo 
utasambaza maji ya kutosha.
chanzo: Mwananchi